Home Kitaifa Kwani Ally Ally ananini na Yanga?

Kwani Ally Ally ananini na Yanga?

5097
1

Kwa mara nyingine tena beki wa KMC Ally Ally amehusika katika kuamua mchezo unaoihusisha timu yake dhidi ya Yanga.

Ally Ally amejikuta mchezaji mwenye bahati mbaya kila anapocheza dhidi ya Yanga, leo March 10, 2019 amejifunga kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara na kuifanya Yanga kushinda mchezo huo kwa magoli 2-1.

Mchezo wa raundi ya kwanza msimu huu uliochezwa October 25, 2018 Ally Ally alimchezea rafu Heritier Makambo nje kidogo ya box la penati ikiwa ni dakika ya 89 ya mchezo na kupelekea Feisal Salum kuifungia Yanga bao pekee katika mchezo huo kwa mkwaju wa adhabu ndogo.

Kumbukumbu zinaonesha July 10, 2018 Ally Ally wakati akiwa Stand United ya Shinyanga aliwahi kujifunga kwenye mchezo ulioihusisha timu yake dhidi ya Yanga. Ally Ally alijifunga wakati akijaribu kuokoa krosi iliyopigwa na Yusuf Mhilu.

Mambo kama haya ni kawaida kwenye mchezo wa soka, inawezekana Ally Ally huwa anakamia kufanya vizuri kwenye mechi dhidi ya Yanga lakini madhara ya kukamia mechi wakati mwingine husababisha afanye makosa mengi.

Kuna wakati fulani Nemanja Vidic alikuwa na wakati mgumu kwenye mechi za Manchester United dhidi ya Liverpool, kama mechi 4 mfululizo ilitokea anaburuzwa na Torres na kushindwa kumzuia kufunga magoli.

Comments

comments

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here