Home Kitaifa Kwa nini ushindani umeshuka kwenye ligi yetu?

Kwa nini ushindani umeshuka kwenye ligi yetu?

2994
0

Baada ya timu zetu za Tanzania (Simba, Yanga, Singida United na Mbao FC) kushindwa kufika fainali ya SportPesa Cup wadau wengi wanasema huenda ligi yetu haina ushindani wa kutosha ukilinganisha na Kenya.

Inawezekana ligi ya Kenya ipo juu kwa sababu kwao klabu yoyote ina nafasi ya kushinda ubingwa wa ligi lakini hapa kama sio Yanga basi ni Simba ushindani kutoka kwa vilabu vingine ni mdogo ukiitoa Azam.

Tumekwama wapi?

Uchumi ni namba moja kwa sababu enzi hizo ukizungumzia level ya ushindani ukiangalia timu ambazo zilikuwa zinapambana Pamba wakati ule ilikuwa chini ya mamlaka ya Bodi ya Pamba, Biashara Shinyanga, RTC Kigoma, Pilsner, Sigara na vilabu vingine vingi vilikuwa vinamilikiwa na taasisi.

Vilabu vya wanachama pia vilikuwa vina nguvu kama Coastal Union, African Sports na mfumo wa ushindani ulikuwa unavifanya na vyenyewe viwe imara kutokana na uimara wa timu za taasisi.

Wakati huo wachezaji walikuwa hawapati pesa nyingi kama siku hizi, walichokuwa wananufaikanacho ni ajira. Ukisajiliwa kwenye timu ya kampuni tayari unajihakikishia ajira ya kudumu.

Baada ya makampuni kuamua kuziachia timu zijiendeshe zenyewe, hapo ndipo mambo yalipobadilika.

Nyakati hizi ni tofauti na enzi hizo, sasa hivi tunahitaji ubunifu wa hali ya juu, ili kukabiliana na maisha ya sasa huhitaji tena kuishi kizamani unatakiwa uishi kulingana na mahitaji ya sasa. Tunahitaji nguvu ya ziada.

Ukiangalia Kenya timu zao nyingi bado zipo chini ya taasisi kwa mfano Ulinzi, Bandari, Tusker, Sony Sugar, KCB, kwa hiyo inawezekana ushindani kwenye ligi ni mkubwa kwa sababu ya timu zao kumilikiwa na taasisi.

Wachezaji wengi wa hizo timu wana uhakika wa kupata mishahara yao kwa wakati kwa hiyo wanacheza mpira wakiwa awana mawazo ya njaa kichwani.

Changamoto waliyonayo kwenye soka la Kenya ni kupoteza mashabiki lakini ndani ya uwanja kuna ushindani mkubwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here