Home Brazuka Kitaani Kushuka daraja sio kufa.

Kushuka daraja sio kufa.

4133
0

Mwishoni mwa msimu wa mwaka 2016-17, Sunderland AFC ilishuka daraja kutoka ligi kuu ya uingereza kwenda ligi ya daraja la chini yaani Sky Bet Championship league. Tukumbushane majina ya wachezajazi na tujiulize kipi kilienda kombo?.Hapa tunamzungumzia mlinda mlango Jordan Pickford sasa yupo Everton Fc, Jason Denayer sasa ni mlinzi wa kati ya Lyon ya ufaransa, Javier Manquillo kwa sasa anakipiga Newcastle, Lamine Koné yupo kwa mkopo Strasbourg ya Ufaransa, Patrick Van Aanholt yupo Crystal Palace Uingereza, Wahbi Khazri yupo Saint-Étienne ya Ufaransa, Adnan Januzaj anaekipiga Real Sociedad Hispania, na washambuliaji mahiri Fabio Borini ambae yupo AC Milan ya Italia na mfungaji bora wa sunderland kwa msimu huo Jermain Defoe ambae yupo AFC Bournemouth.Je ni ule usemi wa kwamba unapoanza safari wengi wanakutia moyo, na unapotaka kuonesha mafanikio wanaibua vikwazo?. Mtawanyiko wa wachezaji hawa ukasababisha sunderland kuzama zaidi na kushuka mpaka Ligue 1 ya nchini hapo, ambapo anakutana na klabu ya akademi ya Manchester city katika michuano ya EFL trophy inazohusisha timu zinazocheza ligi 1 na 2 nchini humo, waweza kuita Manchester city C.Pamoja na magumu hayo yote sasa Sunderland wanaendelea kupambana kurejea walau kucheza Championship kwa msimu ujao, japokua nuru ya njia yao imepotea lakini wanaimani kuwa bado wapo katika njia sahihi.Tunajifunza nini hapo?Turudi miaka ya 1980-90 ya nchini kwetu, mwaka 1986 rekodi iliwekwa na Wanyakyusa wa kutoka Mbeya Tukuyu . Tukuyu stars Ilipanda daraja na kuchukua ubingwa huku ikiwaacha vilabu vikongwe Yanga fc na Simba sports club. Ambapo iliwajumuisha Kocha Mkuu, Athumani Juma, ni pamoja na Mbwana Makatta, Peter Mwakibibi, Michael Kidilu, Assanga Aswile, Godwin Aswile, Michael Kamba, Salum Kabunda na Aston Padon ambaye baadaye alisajiliwa na Simba.Pia mwanzoni mwa miaka ya 1990 kulikua na MECCO iliyopanda na kuleta changamoto kubwa kwenye mpira wa tanzania kiasi cha kuzitia hofu simba na yanga na kukumbwa na kasumba ya kuzaniwa wachezaji wake wanatumia madawa ya kuongeza nguvu. Hapa nawazungumzia Ephraim Kayetta, Nassib Abbas na Jonh Abbas Kanyiki.Pia kulikua na Pamba ya Mwanza ilikua hatari miaka ya 1990-95, ilikua na na wachezaji kama Kipa namba moja Madata Lubigisa, Khalfan Ngasa, Ali Bushiri, David Mwakalebela na Juma Amiri Maftah. Ambayo ilitoa ushindani mkubwa katika ligi kuu ya Tanzania bara. Hao waweza kuwaita Pamba FC au Tout Poisssant Lindanda.Hizo ni baadhi ya timu zilizo tamba miaka ya nyuma hapo, nyingine zilikua Pilsner, Sigara ya Dar-es-Salaam, Ushirika ya Moshi, Reli ya Morogoro na maji maji ya Songea.Baadhi ya vilabu hivi vilivyoitikisa ligi kuu ya Tanzania bara, vipo vinavyo cheza ligi daraja la kwanza na vingine daraja la pili. Na vipo ambavyo vimepotea kwenye ramani ya soka la Tanzania. Bodi ya ligi, shirikisho la soka na wadau wa soka la Tanzania, hebu tujaribu kutupia jicho kwenye ligi daraja la kwanza na daraja la pili, hii ni pamoja na kuepusha janja janja zinazoendelea katika ligi zetu. Lawama za kuwashutumu waamuzi haziishi, vitisho kwa waamuzi, na vurugu za mashabiki kama hatupo nchi ya Tanzania yenye amani vinatia doa ligi zetu.Naamini tukipata mzamini mzuri wa ligi hizi zote tatu, na tukapata maonyesho ya moja kwa moja yaani mubashara, madhambi haya yanaweza kupungua. Na kuwepo uwezekano wa kurudisha maajabu ya miaka iliyopita. Ni wazi pia vilabu vyetu kongwe havija poteza nia na imani za kurudi ligi kuu ya Tanzania bara.Mwandishi : ISACK MSINJILI

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here