Home Kimataifa Kuelekea mechi ya Juventus vs Chievo, tuangalie mechi za kwanza za CR7...

Kuelekea mechi ya Juventus vs Chievo, tuangalie mechi za kwanza za CR7 za ushindani alikopita

9229
0

Juventus vs Chievo ndio mchezo mkubwa sana unaosubiriwa na mashabiki wa soka duniani wikiendi hii, watu wanataka kumuona Ronaldo tu.

Lakini tukiwa tunajiandaa kuuangalia mchezo huu na ligi nzima ya Serie A kupitia DSTV ni vyema leo tukakumbushana mechi za kwanza za ushindani za Cr7 huko alikotoka.

Sporting Lisbon. Hii ilikuwa tarehe 14 August mwaka 2002 katika mchezo wa Champions League kati ya Sporting vs Inter Milan, wafungaji wote vinara wa pande mbili hawakuwepo.

Mario Jardel hakuwepo upande wa Sporting huku Ronaldo De Lima hakuwepo Inter. Cr7 dakika ya 55 aliingia akicheza upande wa kushoto huku kulia akiwa Ricardo Quaresma.

Inter walionekana bora kuliko Sporting na hadi mpira unaisha Cristiano Ronaldo na wenzake walikufa kwa mabao 2-0 na mchezo wa marudiano kocha akamtosa.

Manchester United. Hii ilikuwa siku kama jana August 16 ambapo Ronaldo aliingia uwanjani dakika ya 61 wakati huo United walikuwa wakicheza mechi ya ligi dhidi ya Bolton.

Mashabiki waliamka kumpigia makofi kijana huyo wa Kireno na hakuwaangusha, kwa dakika takribani 30 alizokuwa uwanjani alitoa mchango wa mabao 3 kwa United.

Alikuwa akiwahangaisha sana mabeki wa Bolton walioongozwa na Nicky Hunt huku Kevin Nolan alipigwa chenga hadi akaamua kumvuta jezi kwenye box ikawa penati, United walishinda 4-0.

Real Madrid. Mchezo wa kwanza wa Cr7 La Liga ulikuwa dhidi ya Deportivo La Coruna August 29 katika mchezo ambao Real Madrid waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-2.

Real walitangulia kupitia Raul Gonzalez dakika ya 26 kabla ya Riki kuisawazishia Deportivo, kisha Ronaldo akafunga bao lake la kwanza La Liga kwa penati na Diarra akaongeza lingine na mchezo kuisha 3-2.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here