Home Kimataifa Kocha wa Yanga AIFUNDA Simba kimataifa

Kocha wa Yanga AIFUNDA Simba kimataifa

4304
0

Kocha wa Yanga Zahera Mwinyi ametoa ushauri kwa Simba ambayo ipo Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kucheza dhidi ya AS Vita katika ligi ya mabingwa Afrika.

“Kitu ambacho naweza kuishauri Simba, hawatakiwi kucheza kama walivyocheza hapa na timu kutoka Algeria (JS Saoura). Ile timu ilikuja hapa kutafuta matokeo ya sare lakini mechi ikamalizika wakiwa wamefungwa 3-0.”

“Simba ni timu nzuri, wameenda Congo wanatakiwa wacheze mpira siku hizi hakuna mambo ya nyumbani wala ugenini. Unaweza kuwa na lengo la kushinda ugenini na nyumbani au kuamua kujilinda kupata matokeo ya 0-0.”

“AS Vita ilifungwa mechi ya kwanza ugenini, kwa hiyo itakuwa inacheza nyumbani sehemu ambayo itakuwa na presha ya mashabiki, Simba wanatakiwa kuwa watulivu wasifanye makosa mengi au wakasabisha penati itakuwa tatizo.”

“Kwa sababu wanawachezaji wazuri wanaweza kuamua kucheza wanaweza kupata goli, huo ndio ushauri wangu. Nimeshasema tangu zamani hakuna timu ndogo wala kubwa.”

Kumbuka kocha wa AS Vita Florent Ibenge ndio kocha mkuu wa timu ya taifa ya DR Congo, halafu Zahera Mwinyi ni msaidizi wa Ibenge timu ya taifa!

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here