Home Dauda TV Kocha wa Lipuli kafunguka ushindi wa Simba…kamtaja refa na wachezaji

Kocha wa Lipuli kafunguka ushindi wa Simba…kamtaja refa na wachezaji

5231
0

Kocha msaidizi wa Lipuli FC Selemani Matola kabla ya game yao dhidi ya Simba alisema amechowa na matokeo ya sare ambayo timu yake imekuwa ikipata dhidi ya Simba na leo aliahidi kuibuka na ushindi lakini mambo yamekwenda tofauti.

Simba imevunja rekodi ya Lipuli kuibania Simba kwenye mechi za ligi ambapo kabla ya ushindi wa leo, Simba ilikuwa haijashinda mbele ya Wanapaluhengo kwenye mechi tatu zilizopita.

Baada ya Lipuli kuchapwa 3-1 leo wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, Matola amesema ni matokeo ya mchezo lakini safu yake ya ulinzi imeruhusu magoli mepesi sana.

“Makosa yaliyofanywa na defence yangu yamepelekea turuhusu magoli mepesi sana kwa Simba”-Selemani Matola.

Katika kipigo hicho Matola amesema kiufundi walikuwa vizuri zaidi ya Simba lakini pia amemtaja mwamuzi wa mchezo wao aliwanyonga.

Hapa chini unaweza kuangalia interview ya kocha wa Lipuli Selemani Matola  wakati anazungumza na Dauda TV kupitia YouTube…Bonyeza PLAY▶uiangalie mwanzo mwisho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here