Home Kitaifa Kocha wa Biashara apongeza wa Stand aponda waamuzi

Kocha wa Biashara apongeza wa Stand aponda waamuzi

3059
0

Biashara United imeendeleza ushindi kwenye uwanja wak wa nyumbani (Karume, Musoma) kwa kuifunga Stand United bao 1-0 kupitia Waziri Junior.

Kocha wa Biashara Amri Said amewapongeza Stand, wachezaji wa timu yake na benchi zima la ufundi.

“Nawapongeza Stand United wamecheza vizuri, waamuzi na wachezaji wangu kwa kucheza vizuri na kupata matokeo”-Amri Said, kocha Biashara United.

Kocha wa msaidizi wa Stand United Athumani Bilali ‘Bilo’ amewaponda waamuzi waliochezesha mchezo huo.

“Mechi ilikuwa ngumu tumecheza vizuri kwa dakika 80 lakini tumekuja kupoteza mechi kwa maamuzi ya waamuzi. Mpira haukuwa sawa kuanzia dakika ya kwanza hadi 80 na mwamuzi ndio ameamua matokeo”-Bilo.

“Sijawahi kuona kiwanja chenye matatizo kama mechi ya leo  hadi polisi wanaingia uwanjani kufanya fujo. Kama tunataka mpira wa Tanzania uendelee hii hali iishe.”

“Baada ya Biashara kupata goli ball boys hawana tena mipira, tumetumia mpira mmoja hadi mwisho. Hatukatai kufungwa lakini mpira uchezwe uonekane.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here