Home Kitaifa Kitendaliwa cha Mdhamini mkuu TPL nani atategua

Kitendaliwa cha Mdhamini mkuu TPL nani atategua

2505
0

Tunapokuwa tunacheza mchana kutwa mitaani, tukumbuke pia na wapi tutakula ikifika jioni. Tuangaze macho penye ukungu ili tuweze kukabiriana na jambo litakalo tukumba. Tanzania premier league (TPL) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) ni kama baba na mwana. Mototo akiwa TPL na baba TFF.Mnamo msimu 2015/16, ligi ya uingereza ilipoteza udhamini wa ligi kutoka kwa kampuni ya kibenki Barcleys Bank hivyo kufanya ligi hiyo kupoteza muhimili muhimu wa uendeshwaji wa ligi hiyo. Ambapo benki hiyo ilikua ikitoa huduma ya udhamini kwa mshindi wa ligi kwa takribani miaka 23.Lakini kwa sasa Barclay’s wanabaki kuwa kama wadhamini wa kitengo cha tatu, hii ni baada ya kampuni ya nike kuwa mdhamini rasmi wa mipira na EA sports kama mshiriki katika Nyanja ya tekinolojia. September 2018 kampuni ya vinywaji Coca-cola wakakubali kuwa wadhamini wakubwa wa ligi hiyo. Kufanya jumla ya wadhamini saba.Wakiwemo Barcleys, Carling, Cadbury, Nike, Tag Heuer, na EA Sports. Hivo kufanya ligi hiyo kuendelea bila kuwa na wasiwasi. Na bingwa wa mwaka 2017/18 kupatiwa kitita cha £150 milioni.Msimu wa 2018/19 TPL imeanza kwa kushirikisha timu 20 kwa mara ya kwanza. Hii inahusisha timu tofauti kutoka mikoa zaidi ya kumi na tatu.Kwa sasa ligi hii haina mdhamini mkuu wa mashindano na hili linafanya kuwa kitendawili kisicho kuwa na jibu. Hasa pale maswali kama ‘Bingwa wa msimu huu atapata nini?’. Si hivyo tuuh je! hali za vilabu vyetu zipoje?, hii haimanishi kwamba TPL ni bora sawa na ligi ya uingereza. Lakini je tufanye nini ili tuweze kufikia pale tunapo ota kuwa tutafika.Nini kifanyike? , Kwanza, ni kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji yatakayo wavutia, pili ni kujitangaza katika mitandao mbali mbali ya kijamii na internet, tatu ni kuwa sahihi na ratiba za mashindano zisizo ingiliana na mashindano nje ya ligi, pia mawasiliano mahusiono mazuri na mashirikisho mengine makubwa kama FIFA, CAF n.k.Mwisho ni kuepuka uswahili na mazoea na kufanya kazi kitaaluma. Shirikisho la mpira wa miguu linajitahidi kwa upande wake lakini pia kuna mapungufu yanayo jitokeza. Kwa kuzingatia haya hata kile kidogo tulikua nacho tunaweza kufanya makubwa mengi. Hata sisi pia tunaweza fikia walipo Laliga , Serie A na wengineo.MWANDISHI : ISACK MSINJILI

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here