Home Kitaifa Kipanya yupo tayari uongozi Yanga, yumo pia kuchangia

Kipanya yupo tayari uongozi Yanga, yumo pia kuchangia

3765
0

Hivi unajua kuwa Masoud Kipanya ni shabiki ‘lialia’ wa Yanga? Kupitia kipindi cha Nyundo ya Baruan Muhuza aliuzwa kama yupo tayari siku moja kuja kuiongoza klabu hiyo au shirikisho la soka nchini TFF.

“Shirikisho la soka (TFF) hapana, Yanga kwa sababu ya kuunga mkono siwezi nikasema kwamba nitakataa ingawa sipendi kuwa kiongozi naona hapa nilipo ni patamu sana.”

“Hakuna kitu kizuri kama kazi yako ikiwa kukosoa na kurekebisha, lakini kwa ninavyoipenda Yanga ikitokea nafasi ya kuiunga mkono kwa mfumo wowote ule sina hakika sana kama nitakataa.”

“Najua tunapitia kipindi kigumu sana, lakini sina wasiwasi najua tutavuka.”

Kama unavyojua, kwa sasa Yanga haiko sawa kiuchumi na imekuwa ikitumia mifumo mbalimbali ya kuchangisha mashabiki wake. Masoud huwa anaichangia Yanga?

“Hatusemi tu kwenye mifumo ya kuchangia kupitia simu huwa tunachangia kiasi gani, kwa hiyo huwa tunachangia huko chinicbini.”

#Source: Nyundo ya Baruan Muhuza @azamtvtz

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here