Home Kitaifa KIOJA LIGI KUU! Mchezaji apoteza fahamu uwanjani hakuna AMBULANCE

KIOJA LIGI KUU! Mchezaji apoteza fahamu uwanjani hakuna AMBULANCE

3032
0

Bado hali ya usalama viwanjani inaonekana si shwari au hauzingatiwi, inawezekana wakati huu tungekuwa tunaongea habari nyingine baada ya kukosekana kwa gari maalum la kubeba wagonjwa (AMBULANCE) kwenye uwanja wa CCM Kirumba wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara Mbao FC vs Coastal Union.

Mchezaji wa Coastal Union Adeyum Saleh alianguka ghafla uwanjani na kupoteza fahamu.  Adeyum ilibidi abebwe kwenye gari binafsi (Harier) ili kuwahishwa kituo cha afya baada ya kupatiwa huduma ya keanza.

Daktari wa Costal Union Kitambi Mganga ameeleza sababu ambayo imepelekea mchezaji huyo kuanguka wakati mchezo unaendelea.

“Tatizo ni upungufu wa maji kwa sababu wachezaji wanapoteza maji mengi kwa kuvuja jasho na hii wakati mwingine husababishwa na kucheza wakati wa jua kali”-Kitambi Mganga, daktari Coastal Union.

Mchezaji mwenyewe (Adeyum Saleh) amesimulia ambacho kilimtokea kabla ya kuanguka uwanjani na kupoteza fahamu.

“Sijui ni nini. Mechi za saa 8 mchana nimeshacheza mara nyingi na bado naendelea kucheza lakini leo sijui nini kimetokea. Nilihisi miguu imekosa nguvu nikaanguka lakini namshukuru mchezaji mwenzangu wa Mbao kwa kuniokoa”-Adeyum Saleh.

Mchezaji wa Mbao FC Rafael Siame ndiye alikuwa karibu na Adeyum wakati akianguka na kupoteza fahamu, aliingiza mkono kwenye kinywa cha Adeyum na kumsaidia baada ya kuona anang’ata ulimi.

“Huyu ni ndugu yangu japo ni timu tofauti lakini tunaangalia utu zaidi. Alivyoangu nilikuwa wa kwanza kufika kwa sababu niliona anang’ata ulimi nikaweka mkono wangu kwenye kinywanchake ili kumsaidia”-Rafael Siame, mchezaji Mbao FC.

“Sijawahi kupitia mafunzo yoyote ya huduma ya kwanza lakini nilijikuta nikimsaidia kwa sababu nilikuwa wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio.”

Kocha wa Coastal Union ameelekeza lawama zake kwa wapangaji wa ratiba ambapo mchezo huo awali ulikuwa uchezwe saa 10:00 jioni lakini ukarudishwa nyuma hadi saa 8:00 mchana huku akieleza tukio la mchezaji wake kuanguka uwanjani.

“Sioni sababu za mechi kuchezwa saa 8 mchana kama kuna mazingira ya kucheza saa 8 sawa lakini kwa mazingira yaliyopo sasa hivi ni mateso kwa wachezaji kwa sababu hutaona kiwango”-Juma Mgunda, kocha Coastal Union.

“Kijana wangu amepata rapsha ulimi ulikuwa unakwenda ndani.”

Tukio la Adeyum Saleh kuanguka uwanjani lilitokea dakika ya 46 kipindi cha kwanza, inaelezwa Ambulance ilifika uwanja wa CCM Kirumba zaidi ya dakika 15 baada ya tukio hilo kutokea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here