Home Dauda TV Kinda la Ndondo lilivyoagwa kabla ya kwenda Uturuki

Kinda la Ndondo lilivyoagwa kabla ya kwenda Uturuki

3297
0

Mchezaji Rabbin Sanga wa kituo cha Bombom Youth aliagwa January 31, 2019 kabla ya kwenda kufanya majaribio ya siku 10 kwenye klabu ya Besiktas ya Uturuki.

Sanga mwenye umri wa miaka 15 amepata nafasi hiyo baada ya kuibuka mchezaji bora wa michuano ya Ndondo Cup Academy inayoandaliwa na Clouds Media Group kwa kushirikiana na DRFA kupitia kipindi cha michezo cha Sports Xtra.

Hafla ya kumuaga mchezaji huyo imefanyika maskani ya kituo hicho yaliyopo Kariakoo mtaa wa Twiga na Jangwani na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwepo Mwenyekiti wa DRFA Almasi Kasongo na wadhamini wa michuano hiyo kampuni ya Beko.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here