Home Kitaifa Kinachoitesa Yanga sio Ukata, ni tamaa na hela za Manji

Kinachoitesa Yanga sio Ukata, ni tamaa na hela za Manji

5147
0

Yanga waliishi miaka 11 kitajiri. Walikuwa wanakula pesa za Manji kama zao tu. Wakasahau mtegemea cha ndugu hufa masikini. Klabu iliendeshwa kwa fujo fujo za hela za Manji, walikula kama zao vile. Walisajili mastaa kibao kutoka nje n.k. Walilitawala soka haswa. Hakuna mchezaji aliyelia njaa.

Lakini hawakujali sana kuhusu kesho.

Ilipofika nyakati za mabadiliko kila mtu alianza kuthamini kijiko chake. Manji hakutaka kupewa timu kwa kura za watu, alitaka kupewa timu kwa sababu ana hela, hehe hehe, nani angekubali? Wakimpa timu wao watakula wapi? Waache kuitwa walezi wa Yanga wakaitwe vibaraka wa Manji!!!.

Wapo waliomtaka Manji asimame kama mwenyekiti na kama mwekezaji. Lakini kama akikubali kuwa mwenyekiti lazima aongozwe na katiba. Yaani atoe hela na bado awe chini ya maandishi yaliyotungwa na watu ambao walilipwa mshahara kwa fedha zake, tehe tehe.

Yule ni mfanyabiashara, lazima aangalie maslahi yake. Alipoona mzozo uanzidi Manji aliwaambia chagueni mwenyekiti mimi nitamshauri. Manake alijitoa kabisa kwenye suala la kusikiliza maoni ya watu ndani ya klabu namna gani watumie fedha zake.

Kimsingi ukiwa mwenyekiti lazima uwe chini ya katiba, lazima ukubali kufuata taratibu zilizopo. Kwa namna nilivyomuona Manji hataki hayo maisha. Anataka kuwa boss na Yanga iwe mali yake.


Ni fedha zangu halafu leo nipangiwe na watu ambao nawalipa mimi?


Wenzetu ulaya wananunua timu, halafu wanaweka wakurugenzi ambao lazima wasikilize matakwa yao.

Na mfumo wa hisa bado Manji angenunua hisa nyingi na bado angekuwa na mamlaka na timu. Hapa kidogo mgonjwa angetafuniwa maji kuokoa maisha yake.

Manji anasubiri jambo ambalo wenye tamaa wengi hawajamuelewa. Mfumo wa kisasa wa uendeshaji timu. Ununuzi wa hisa. Hapa ndipo Manji atakuwa na rungu sahihi la kuiongoza Yanga anavyotaka. Mwisho wa siku anajua hakuna atakayemzidi manunuzi ya hisa. Manji hataki cheo anataka timu, wanachamana wanamtaka Manji na timu pia. Kama wanaitaka timu waige mfumo wa wenzao Simba. Wasikimbilie kumendea fedha za Manji tu wakati zao wameficha ndani.

Manji alikuwa anawinda cheo cha juu cha mwisho ndani ya klabu kwa muda mrefu. Cheo cha uenyekiti sio cheo kama kuna mmiliki. Atakuwa mpiga debe wa mwenye timu tu.

Tukiachana na sakata la Manji na hela zake

Huyo atakayechaguliwa kuwa mwenyekiti anapaswa kujua kitakachomfanya awe na thamani ndani ya klabu ni mipango thabiti ambayo itamfanya mwekezaji asiwe na nguvu kuizidi timu.

Wanayanga wengi walikuwa wanamlilia Manji awe mwenyekiti, je huo uenyekiti utamsaidia nini? Mtu anawapa hela halafu mnamhonga uenyekiti? Hana shida na hicho cheo chenu. Yeye anawaza ni kwa namna gani atatengeneza klabu kubwa inayomlipa mamilioni ya fedha na sio kamshahara kenu ka uenyekiti. Mwisho wa siku mshahara wa uenyekiti unatoka mfukoni kwake.

Nikumbushe tu, Yanga haihitaji fedha pekee, inahitaji mfumo imara wa mapato. Mkiweka viongozi ambao hawana mipango thabiti matatizo hayataisha. Tumeona viongozi wanasema tu mfumo wa kisasa lakini hakuna hata mmoja aliyeainisha njia mpya na madhubuti za kupata mapato. Wote wataishia kusema logo ya klabu (mauzo ya jezi).

Pato kubwa la klabu ni mashabiki. Mashabiki kupitia gate collections (ticket). Ukweli ni kwamba wingi wa mashabiki uwanjani ni fursa kubwa kwa wawekezaji, na mauzo ya TV. Sio lazima mechi zao zioneshwe na Tv moja wanaweza kusema hatutaki mechi za Hapa Dar taifa zisioneshwe ili mashabiki wetu wa Dar waje kwa wingi uwanjani, au wanaweza kusema hatutaki mtu auze maji pale taifa tutaleta maji yetu ya jangwani tuuze. Hakuna hata mmoja aliyekuja na mikakati ya kupata hela mipya. Ovyo kabisa. Enewei uchaguzi mwema ila msilete vurugu tu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here