Home Kitaifa Kiemba aponda ushirikina Azam

Kiemba aponda ushirikina Azam

4438
0

Kupitia #SportsRoundUp ya Clouds FM kulikuwa na mjadala kuhusu matukio kadhaa yanayohusisha imani za kishirikina yaliyojiokeza kwenye mchezo wa Azam vs Simba.

Mchezaji wa zamani aliyepita vilabu vya Kagera Sugar, Yang, Simba, Azam na Stand United Amri Kiemba ame-share experience yake kuhusu matukio ya aina hiyo.

“Sasa hivi inaonekana haya mambo kama ndio yameanza kwa sababu yanamulikwa sana na vyombo vya habari lakini yapo kitambo tu. Kwenye timu zote nikizocheza sikupata bahati ya kucheza timu ambayo hawafanyi hivi vitu zaidi ya Azam.”

“Wakati nacheza Azam kulikuwa hakuna hayo mambo baada ya mazoezi mnapewa maelekezo ya mechi mnaingia kucheza mambo mengine kama yalikuwa yanafanyika basi wachezaji walikuwa hawajui wala hawashirikishwi.”

“Kwingine kote mchezaji ndio mhanga namba moja wa kushiriki uwe unataka au hutaki, na ukikataa unakuwa adui unaonekana sio mwenzio.”

Ni vitu ambavyo havitusaidii, tunashindwa kuwekeza kwenye vitu ambavyo vitatupa ushindi tunakimbilia shortcut.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here