Home Kitaifa Kibonde alikuwa fundi wa Basketball

Kibonde alikuwa fundi wa Basketball

3016
0

Enzi za uhai wa mpendwa wetu Ephraim Kibonde alikuwa ni mwanamichezo haswa na alikuwa vizuri kwenye kuucheza mpira wa kikapu kama ambavyo anaelezea Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania (TBF) Phares Magesa.

“Ndugu yetu Ephraim Kibonde alikuwa mchezaji mzuri wa Basketball Tanzania, wengi tunakumbuka alianza kucheza akiwa mdogo baadaye akajiunga na shule ya sekondari ya Mzizima ambapo alichezea timu ya shule katika ngazi ya UMISETA”-Phares Magesa.

“Baada ya kumaliza sekondari alijiunga na kituo cha vijana cha Don Bosco Upanga ambapo alikuwa mchezaji wa timu ya kituo hicho (Don Bosco) wakati huo timu yao ilikuwa ikicheza ligi daraja la pili.”

“Kibonde alikuwa mchezaji mahiri wa timu hiyo ambapo mchezo unaokumbukwa sana katika timu hiyo ni ule ambao Kibonde alitoa pasi ya mwisho ‘assist’ ambayo ilipokelewa na Dr. Marwa ambaye alifunga pointi 3 na kuiwezesha timu yao kupanda daraja hadi daraja la kwanza.”

“Mchezo wa mwisho ambao mimi pia nilimshuhudia akicheza ilikuwa mwaka jana kabla ya FIESTA 2018 mchezo uliofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana ambapo timu ya Clouds Media Group ilicheza na wasanii wa burudani Tanzania.

“Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania tunasikitika sana tumempoteza mwenzetu, tunatoa salam za pole kwa familia yake, Clouds Media na wote walioguswa na msiba huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here