Home Kimataifa Kevin Boateng kutua Barcelona

Kevin Boateng kutua Barcelona

3940
0

Kama kuna habari imeteka vichwa vya habari kule ulaya ni habari ya Boateng kwenda Barca. Nyota huyo wa zamani klabu ya AC Milan Kevin Prince Boateng anatarajia kufanya usajili wa kushtukiza sana kutua Barcelona.

Boateng ambaye kwa sasa anacheza kunako klabu ya Sassuolo anatarajia kutua Camp Nou kwa mkopo. Wengi wanajiuliza kuna nini? Kwanini Boateng? Atacheza nafasi gani? Yale yale ya akina Paulinho na Turan au kuna kitu cha tofauti kwake?

Barcelona imeingia makubaliano ya kumnunua moja kwa moja hapo baadae kwa dau la £8.

Je ataweza kupigania namba pale Camp Nou au amekwenda kula pensheni?

Mkurugenzi wa ufundi wa Sassuolo anatarajia kusafiri kwenda mpaka kunako jiji la Barcelona kukamilisha dili hilo.

Thamani ya mkopo huo inafikia £2M. Kevin Prince Boateng(31) amecheza vilabu kadhaa kama vile Hertha Berlin, Tottenham, Dortmund, Portsmouth, Milan, Schalke 04, Milan, Las Palmas, Frankfurt, Sassoule.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here