Home Kimataifa Karibu Kwenye Ulimwengu Mpya Wa Stephen Curry.

Karibu Kwenye Ulimwengu Mpya Wa Stephen Curry.

4162
0

Inawezekana mchezaji Stephen Curry akawa ni mchezaji anayependwa zaidi kwa sasa kwnye NBA na anaendelea kujiongezea umaarufu kwa namna ambayo ameweza kubadili fikra za wengi na kufanya mapinduzi kwenye mchezo wa mpira wa kikapu kwa maana ya umuhimu wa matumizi ya pointi tatu.

Hajawahi kutokea shooter bora kumzidi kwenye NBA na historia yake. Ni huyu Curry ambaye anaongoza kwa kuuza jezi kwa miaka miwili mfululizo kwenye NBA akiwaacha wenzie mbali hata baada ya Kevin Durant kuongezeka kwenye kikosi cha Golden State Warriors.

Baada ya kuonekana kama hatoweza kufanikiwa kuishi vyema kwenye NBA kutokana na majeraha ya kila mara, NIKE waliamua kuachana nae na akachukuliwa na kampuni ambayo bado ilikuwa inakua ya Under Armour.

Image result for curry 2

Maisha yalibadilika kwa kasi sana kwani tangu msimu wa 2014-2015 alikuwa hashikiki kwenye mauzo ya viatu vyake na 2015-2016 akawa mchezaji aliyeuza zaidi akiwazidi Kyrie Irving, Durant na Kobe kwa pamoja. Hii ilikuwa ni katika matoleo ya Curry 1 mpaka Curry 2.

Wabunifu wa viatu kwa Under Armour ni kama walijisahau kwani toleo la Curry 3 lilikuwa bovu na likaonekana kutokukubalika kwa wapenzi wengi wa mchezo wa mpira wa kikapu ikizingatiwa viatu vingi vya Curry ni shingo ndefu, huku wavaaji wengi wakipendelea shingo fupi. Kwenye mauzo ya maduka ya vifaa vya michezo vilikuwa haviuziki kiasi cha Under Armour kuamua kushusha bei maradufu.

Image result for curry 4

Katika kuona hali si shwari Curry hajaamua kuumaliza msimu kimya. Kwenye fainali za NBA zinazoendelea ambazo Warriors wanaongoza 2-0 Curry ameamua kuzindua viatu vyake vipya vinavyoitwa Curry 4s. Sneakers hizi bado hazijaingia sokoni lakini Curry alizitambulisha rasmi kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Cavs na anaweza kufurahi sasa kwani washabiki wake na wengine wamevipokea vyema kweli.

Curry amesemekana kuwa hakufurahia kabisa kitendo cha viatu vyake kushuka kwa kiasi kikubwa thamani na kutokuuzika na hivyo kipindi hiki akaamua kusimamia kuanzia idea mpaka utengenezwaji wake mwenyewe na hakutaka kusubiri mpaka mwisho wa msimu huu au msimu ujao bali akataka kuvitumia kwenye fainali za NBA jambo ambalo Under Armor wamefanya.

Mpaka kufikia fainali za mwaka jana wakati Curry akitumia Curry 2, katika miezi 12 alikuwa ameizalishia kampuni ya Under Armour zaidi ya dola za kimarekani milioni 200 yeye peke yake. Lakini zilipoingia Curry 3 hali ikawa sio shwari hasa pia kutokana na bei yake ya dola 140. Curry na Under Armour kwa pamoja wanategemea viatu hivi (Curry 4) kufanya vyema jambo ambalo linaonekana litafanikiwa. We unavionaje msomaji?

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here