Home Ligi EPL KANTE ANAVYOTEMBEA KWENYE KIVULI CHA PATO NGONYANI

KANTE ANAVYOTEMBEA KWENYE KIVULI CHA PATO NGONYANI

1336
0

Generated by IJG JPEG Library

Kuna wakati mwingine jitihada zinafichwa kwa mgongo wa watu wengine hasa wanaoangaliwa sana na jamii inayowazunguka.kila, shabiki wa mpira duniani ameshangazwa na timu ya Leicester City jinsi ilivyokuja kwa kasi kiasi cha kuvishusha vilabu vikongwe vilivyokuwa vikitawala soka la pale Uingereza.

Nani aliipa nafasi mwanzoni mwa msimu kama wangeongoza ligi hadi kufikia mechi 30 wana kikosi chenye thamani ndogo kulinganisha na Manchester City wanaoshika nafasi ya nne mpaka sasa.

Nani alitegemea kikosi cha West Ham ambacho misimu iliyopita ilikua ikigombania kujinusuru kushuka daraja leo hii wapo nafasi nzuri ya kucheza mashindano ya UEFA.

Leo katika kikosi cha Leicester City kuna wachezaji wanaoongelewa sana,Mahrez na Vardy ni wachezaji wanaoonekana kama kuibeba Leicester wanasahau kuna kijana wa Kifaransa mwenye umbo dogo si mwingine ni Ng’olo Kante kijana huyu kafanikiwa kuwafunika viungo wengi katika ligi ya EPL kivutio kikubwa ni staili yake ya ukabaji.

Ana thamani ndogo kulinganisha na kina Fernandinho wa Man City Coquelin wa Arsenal. Kante aliyesajiliwa kutoka club ya Caen kwa dau la 5.6m lakini ameweza kuonesha kuwa thamani yake imepanda. Kante ndiyo amekuwa akiunganisha vyema safu ya ulinzi ya Leicester City inayoongozwa na Huth na Morgan lakini mashabiki wengi wamekua wakiwaangalia kina Mahrez na Vardy wakimsahau kijana huyu ambaye Sir Alex Ferguson anamwona kama mchezaji bora wa msimu huu.achana na Kante ambaye ni kama kivuli chake kinatembea pale Jangwani.

Timu ya Yanga msimu huu imekua ikifanya vizuri mashabiki wengi wanawaangalia zaidi Kamusoko,Ngoma, Tambwe na hata Kaseke Deus kama nyota wanaoibeba Yanga lakini kuna kijana mmoja anasahaulika kwa mashabiki si mwingine ni Pato Ngonyani.

Pato hufanya kazi ya ziada na kwa upande mwingine ndiyo hurahisisha kazi ya Kamusoko kumiliki dimba. Ngonyani alisajiliwa miaka miwili iliyopita akitokea katika club ya Majimaji ya Songea amefanikiwa kuonesha kipaji alichonacho kulinganisha na umri wake.

Alianza kufanya vizuri na kikosi cha Van Pluijm katika mashindano ya Mapinduzi dhidi ya Azam alipochezeshwa kama beki wa kati, kiraka huyu pia alichezeshwa kama kiungo katika mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba alifanikiwa kiasi kikubwa kudhibiti mashambulizi ya Simba katika eneo hili.

Amekua akikaba kwa utulivu na akili kama ilivyo kwa Kante lakini ni mara chache sana kusikia mashabiki wakimwagia sifa au kumchukulia kama mchezaji anaeibeba timu kama ilivyo kwa Kamusoko.

Ni dhahiri pengo la chipukizi huyu lilionekana katika mechi dhidi ya Azam iliyoisha kwa sare ya goli 2-2 katika mchezo huu Azam walifanikiwa kumiliki sehemu ya kiungo iliyokuwa ikiongozwa na ‘Migi’ na Himid Mao kama angeweza kupewa nafasi angeweza kusaidiana vyema na Kamusoko kuwadhibiti viuongo hawa wa Azam.

Sasa ni wakati wa Pato Ngonyani kuaminiwa na mashabiki wa Yanga na soka kwa ujumla. Thamani yake ni ndogo ukilinganisha na wachezaji wengine lakini kadri anavyopewa nafasi ndivyo thamani yake huongezeka. Hana tofauti sana na Kante ambaye sitoshangaa kuona timu kubwa zikimwekea dau mezani mwishoni mwa msimu huu huku thamani yake ikipanda kwa kasi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here