Home Ligi LIGUE1 Kama Neymar hajamuelewa Ronaldo hatawaelewa waarabu

Kama Neymar hajamuelewa Ronaldo hatawaelewa waarabu

19579
0

Umepata taarifa za Neymar kuwa mchezaji bora ufaransa? Daah hiki ni kioja kingine tena. Ukiacha kituko cha yeye kununuliwa bei ya kisiwa hili la tuzo nalo jambo la kushangaza. Pia nimepigwa na butwaa kwa kauli ya De Lima kwenye ukarasa wake wa Instagram.

Ukiachilia mbali kauli zake za hapo awali, hiki kitendo cha kusifia tuzo ya Neymar kwa nguvu kubwa kiasi kile ni kuonesha wazi ameangalia Zaidi malengo ya Neymar na kiu ya taifa lake kwa ujumla.

Hata mimi kama mdogo wangu nikijua ameibia kwenye mtihani, halafu akafaulu mahafali yake nitaenda na nitamsifia hata maua nitamvalisha.

De lima mwanzoni hakuoneshwa kufurahishwa na maamuzi ya Neymar kwenda PSG kwa kile alichosema kuwa Neymar ameenda ligi ambayo haina ushindani.

Related image

Leo hii Neymar ameshinda tuzo na amejaribu kuelezea kwanini Neymar ameshinda tuzo ile. Ameshasahau.

Mojawapo ya sababu aliyotoa ni kumsifia Neymar kufunga magoli 19 kwenye michezo 20. Maanake amtumia kigezo cha michezo michache. Nimejaribu kujiuliza je Cavan angefunga magoli 15 kwenye mechi 13 kisha Neymar afunge magoli 19 kwenye 20 angemsifia Cavan kwa kucheza michezo michache?

Neymar akilia wakati wa wimbo wa taifa

Bila shaka amejaribu kumbeba Neymar na kuzidi kumpa moyo hasa wakati huu akijiandaa na kombe la Dunia.

Anajua hali aliyo Neymar kwa sasa hasa ukiangalia ametokea majeruhi. Neymar ana mtihani mkubwa sana mbele yake. Hata De Lima mwenyewe anajua ile tuzo sio halali yake lakini ilikuwa muda muafaka kumfikishia ujumbe wake. Huenda alitamani sana kumpa Moyo Neymar na kumuonesha kuwa anaweza kubeba kombe la dunia na huu ndio muda sahihi.

kama Neymar hajamwelewa imekula kwake.

Related image

Binafsi Kuhusu tuzo hii nimeona imebebwa na sababu za kisiasa na kibiashara tu. kwa taarifa yako baadhi ya mataifa ya Kairabu yanaionea Qatar wivu kwa kufanikiwa kiuwekezaji kwenye soka.

Leo hii ukisema kuwa Neymar ni bora kwa sababu amecheza michezo michache na kufunga magoli mengi ni kupaka marashi kwenye kwapa chafu.

Mchezaji ukicheza michezo michache na timu yako ikazidi kufanikiwa hiyo ni sababu kubwa ya kuonesha kuwa hukuwa ukitegemewa.

Related image

Mchezaji usipokuwa na umuhimu mkubwa sana kwenye timu huwezi kupata nafasi ya kuwania hizi tuzo kwa sababu mchango wako upo lakini yule aliyedumu kikosini kwa muda ndiye aliyemwaga jasho kupigania timu yake wakati yeye unakula bata Brazil.

Neyamr alifanya vizuri sawa lakini gubu la Paundi Milioni 222 alizonunuliwa nazo zinatia ukakasi.

Kuna uwezekano mkubwa kununuliwa kwa Neymar ni nguvu ilitoka serikalini. Amini usiamini haiwezekani mtu anunuliwe gharama kubwa kiasi kile halafu leo apewe tuzo kwa sababu dhaifu.

Related image

Kuna uwezekanao mkubwa kabisa kwamba shrikika la soka la ufaransa na Ufame wa Qatar walihusika kwenye kuhakikisha Neymar anapatikana ili kutengeneza mfalme wa kuitangaza ligi yao na Qatar kuzidi kuimarisha biashara zao hasa hasa maandalizi ya kombe dunia mwaka 2022. hapo awali nimesema kuna vita kubwa ya mataifa ya kiarabu kwenye uwekezaji wa soka.

Takwimu za Neymar zinamnyima kabisa hadhi ya kuwa mchezaji bora wa ufaransa

JINA Mechi Hawajafunga dakika asisti Dkk
Neymar 20 8 (20) 2589 6 94
Cavan 32 11 (32) 1797 13 92

Bila shaka tunaona hapo juu kwamba licha ya kwamba Cavan alicheza michezo mingi lakini bado ni michezo mitatu tu aliyomzidi nayo Neymar ambayo hakufunga. Kigezo cha Neymar kucheza michezo michache kinaweza kupingwa na hoja ya kwamba Neymar hata hivyo katika michezo yake hiyo 20 ilitoka kapa michezo nane.

Maanake tukiongeza michezo 12 mbele alikuwa na uwezekano wa kutoka kapa michezo mingine mitano. Katika michezo 26 ya mwanzo ya PSG Neymar alikosekana michezo 6.

Nchi zilizotoa wachezaji bora ndani ya League One

nchi Idadi Mwaka
France
8
1993–94, 1994–95, 1995–96, 2000–01, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2014–15
Brazil
3
1996–97, 2006–07, 2017–18
Sweden
3
2012–13, 2013–14, 2015–16
Belgium
2
2009–10, 2010–11
Portugal
2
2001–02, 2002–03
Argentina
2
2000–01, 2009–10
Ivory Coast
1
2004–05
Ghana
1
2005–06
Italy
1
1997–98
Algeria
1
1998–99
Uruguay
1
2016–17

Hatuwezi kupima pumzi ya mtu aliyekimbia mbio fupi na kumfananisha na aliyekimbia mbio ndefu. Fununu za Neymar kutimkia Madrid zinawatoa udenda wafaransa na Waarabu, waliomwaga pesa zao kumpata Neymar.

Naweza kuamini sasa huenda mawazo ya kumwaga hela nyingi kiasi kile hata hazikutoka kwa mwa mwarabu pekee. Au kuna uwezekano mkubwa mwarabu ana nguvu kubwa katika bodi ya uendeshwaji wa ligi ya Ufaransa.

Qatar wanaandaa kombe la dunia mwaka 2022.

Ufaransa na nchi za ulaya soko lao kiuchumi linadidimia kutokana na kuinuka kiuchumi kwa kasi kubwa kwa China na waarabu. Ufaransa wanakula Chakula na kipofu. hawapaswi kugusa sahani kabisa.

Wanaelewa hasa lengo la Waarabu ni kujitangaza hasa hasa wakilenga zaidi kombe la Dunia. Neymar anatumika kama chambo ili kupata wachezaji wengi wakubwa. Kinachonekana ni kwamba PSG haiwakilishi tena Paris ila ipo zaidi kibiashara.

Wafaransa hawataongelea kabisa hili suala maana wanajua wamejifunika kwenye mwamvuli wa waarabu. Ile ligi ilishajifia. Wao hawashindwi kutoa ndizi ambazo hazijakomaa wakati wanajua wana njaa. taratibu wachezaji wakubwa watajaa Ufaransa

TAKWIMU ZA UJUMLA ZA NEYMAR

Mashindano Magoli Asisti Dakika
LaLiga 123 68 10.015′
Série A 103 54 7.733′
Champions League 47 27 4.037′
Libertadores 25 14 2.243′
Ligue 1 20 19 1.797′
Copa del Rey 20 15 1.711′
Club World Cup 3 1 268′
Copa Sudamericana 2 134′
Supercopa 2 1 121′
Coupe de la Ligue 2 1 180′
Recopa Sudamericana 2 1 180′
Coupe de France 1 2 90′
Jumla 350 2013 28.509

makala hii imeandaliwa na Privaldinho unaweza kunifollow Instagram pia. Makala hii ni mawazo yangu haimaanishi yapo sahihi au

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here