Home Ligi EPL Kabla ya kumshambulia Alvaro Morata wakumbukeni hawa

Kabla ya kumshambulia Alvaro Morata wakumbukeni hawa

13349
0

Morata Morata Morata, kila mtu anapiga kelele kuhusu mshambuliaji huyu wa Chelsea, mashabiki wa Chelsea wamemchoka na sasa wengi wanaona atafute pa kwenda tu.

Morata alijiunga na Chelsea msimu uliopita kwa ada ya £60m akitokea Real Madrid akitajwa kama mrithi wa Diego Costa, lakini kabla ya kumshambulia Alvaro Morata ni vyema tukakumbuka kuna ambao msimi wa kwanza walikataliwa lakini msimu wa pili wakawa lulu.

David De Gea. Wakati De Gea akijiunga na United 2011 kulikuwa na hofu kubwa kuhusu uwezo wake, na kwa kipindi hicho United kulikuwa ndio mabeki wake nguli wanaisha ishia.

Wengi walimsema vibaya De Gea huku wakikadhania kwamba haoni mbali, lakini msimu wa 2013/2014 kila mtu akaziba mdomo na kuamini alikuwa mrithi sahihi wa Van Der Saar.

Patrice Evra. Ferguson alimchukua Evra msimu wa mwaka 2006 kwa ada ya £5.5 akitokea Monaco, msimu ambao United walikufa 3-1 toka City, Evra akaonekana alichomesha akatoswa mchezo na Liverpool huku timu ya taifa nako akapigwa chini.

Lakini katika msimu uliofuata wa ligi Evra pamoja na uwingi wa mabaki waliokuwepo United kama Heinze, Oshea, Silvestre lakini Evra alifanikiwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Ferguson.

Roberto Pires. Wakati Marc Overmars anaondoka Arsenal, Pires alionekana kama mrithi wake Arsenal, msimu wa kwanza tu maisha yake ya ndani na nje ya uwanja yakawa magumu huku Interview aliyofanya akisema alipenda Madrid ila Arsenal alienda kwa sababu ya Wenger ikizidi kumuweka pabaya Gunners.

Msimu wa 2000/2001 ukawa mbovu kwake lakini msimu wa mwaka 2001/2002 Pires alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa chama cha waandishi wa habari za michezo nchini Uingereza.

Michael Essien. Ada ya £24m ilimtoa Lyon kwenda Chelsea mwaka 2005, uwepo wa Frank Lampard, Claude Makelele ulimfanya aonekane sii lolote huku ujio wa Michael Ballack ukampa wakati mgumu kabisa, lakini msimu uliofuata kila kitu kilibadilika kwake na akaanza kuwa kipenzi cha kocha Jose Mourinho.

Javier Mascherano. Wakati anafika tu West Ham mwaka 2006 yeye pamoja na Carlos Tevez wakapoteza mechi 8 na kusuluhu 1, wakati anakwenda Liverpool alinukuliwa akisema “soka ni mchezo wa kuzoea na labda msimu wa kwanza ndio unazoea”, msimu wake wa pili na Liverpool alikuwa kati ya viungo tegemezi akicheza pamoja na Xhabi Alonso na Steven Gerrard.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here