Home Dauda TV Joh Makini amempa jina jipya Lukaku ‘Makaptura’

Joh Makini amempa jina jipya Lukaku ‘Makaptura’

3621
0

Joh Makini amempa jina jipya mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku, wakati Dauda TV inafanya mahojioano na mkali huyo toka kundi la WEUSI alisema Ulaya hakuna timu anayoishabikia kwa sasa bali ni shabiki wa wachezaji wanaofanya vizuri.

Amesema amekuwa akivutiwa na wachezaji wengi wenye asili ya Afrika ndipo akataka kumtaja Lukaku lakini akashindwa kutaja moja kwa moja jina la mchezaji huyo badala yake akasema "Yule makaptura, ambaye siku hizi amekuwa bonge" akimaanisha Lukaku.

Kibongobongo Joh Makini ni shabiki wa Simba wakati mdogoake Nikki Wapili yeye ni shabiki wa Yanga.

Angalia video hapo chini👇kupitia YouTube kwenye channel ya Dauda TV. Bofya PLAY▶kuangalia mwanzo mwisho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here