Home Ligi BUNDESLIGA Jerome Boateng: Sababu kwanini Jay Z anamsaidia beki huyu kuiteka Marekani

Jerome Boateng: Sababu kwanini Jay Z anamsaidia beki huyu kuiteka Marekani

1110
0

Mwezi June, mlinzi wa Bayern Munich na Germany alikuwa mwanasoka wa kwanza kusainiwa kwenye kampuni ya usimamizi wa wanamichezo ya Roc Nation Sports – kampuni iliyoanzishwa na rapper wa kimarekani Jay Z miaka miwili iliyopita.
 
Wawili hao walisherehekea dili hilo katika moja ya klabu za Jay Z – 40/40 Sports Bar huko Manhattan, kabla ya Boateng hajapewa VIP pass kwenda kwenye Mary J Blige.

Mkataba huu wa Roc Nation na Boateng unamaanisha mjerumani huyo atakuwa akitangazwa kibiashara na kutafutiwa fursa mbalimbali ndani ya ardhi ya Marekani kama ilivyo kwa mcheza mpira aa kikapu wa NBA Kevin Durant na mwanasumbwi tajiri Miguel Cotto.

Roc Nation pia kwa upande mwingine inasimamia kazi za kimuziki na biashara za wasanii Kanye West, Rihanna, Rita Ora, Shakira na Jay-Z mwenyewe.
Kwanini Boateng?

Wamerekani wanamuelezea kijana huyu kwa maneno haya: he’s cool.

Ushindi wake wa kombe la dunia mwaka 2014, ushindi wa Champions league na Bayern mwaka 2013, makombe matati ya Bundesliga – rekodi hizi zinamfanya awe miongoni mwa wachezaji wa daraja la juu duniani na hiyo inamfanya au inamuongezea mvuto wa kibiashara.

Roc Nation ilivutiwa na hili – pia Boateng ana ndugu yake mwingine George ambaye ni mwanamuziki wa hip hop ambaye anakuja vizuri kwenye game la hip hop huko barani ulaya. Roc Nation wanaamini kuonekana kwake kwenye video za ndugu yake kunasaidia, pia biashara yake ya kutengeneza miwani za brand yake.  
Pia anazungumza vizuri kabisa lugha ya kiingereza, historia yake ya nyuma inayolandana na maisha ya vijana wa sasa, kujitoa kwake kwa jamii – ikiwemo suala la kuwasaidia wakambizi hivi karibuni akiwa na klabu yake ya Bayern Munich – Roc Nation wanaamini hizi sifa zote zinaongeza thamani yake katika kumuuza kibiashara.

“Jerome ni mmoja wa wachezaji wakubwa duniani. Ni mwanamichezo mzuri, lakini pia ana sifa nyingi za nje ya uwanja zinamuongezea thamani” anaelezea Raisi wa masuala ya branding wa Roc Nation Michael Yormark.

“Anapenda fashion, burudani na music – mambo yanayomfanya awe mwepesi sana kumuuza na yote yanafungua milango ya brands kuja kutaka kufanya nae kazi.

“Ana staili tofauti na swagga zenye kumtanbulisha vizuri, kujiamini kwake pia kunavutia sana.”

*****

Boateng ameboreka zaidi kama mchezaji na binaadamu tangu alipoondoka Manchester City baada ya msimu mmoja.
Baada ya kusajiliwa kutoka Hamburg mwezi June 2010, maisha yake ndani ya City yalianza vibaya wakati alipopata majeruhi mwanzoni tu. Alifanikiwa kucheza mechi 24 tu na mara nyingi alikuwa akichezeshwa nafasi ambayo hakuwa anaimudu – beki a kulia.

Aliposajiliwa na Bayern mwaka mmoja baadae, malengo yake yalikuwa ya wazi kabisa. “Nimekuja hapa kuunda safu ya ulinzi imara zaidi,” alisema.

Na sasa anaonyesha kuwa na njaa zaidi. “America ni soko kubwa. Ni bara lenye mvuto wa kipekee. Tutaona namna nitakavgoweza kukamata fursa,” alisema baada ya kuingia mkataba na Roc Nation.

Ana vitu kidogo sana vya kupoteza – kama hatofanikiwa.

Roc Nation jukumu lao kuu ni kujenga brand ua Boateng ndani ya America.

Katika masuala kujadili mikataba bado anasimamiwa na SAM Sports – kampuni ya kijerumani inayoendeshwa na mchezaji wa zamani wa Bayern Munich Christian Nerlinger.

Roc Nation wameshawahi kufanya kazi kwa namna hii huko nyuma. Wakati ilipokuwa changa ilijiunga na kampuni ya kubwa ya masuala ya ngumi ya Creative Artists Agency – ambao pia wanamuwakilisha Cristiano Ronaldo – kuanza kufanya kazi na soko la Creative Artist kuliisaidia kujijenga kitaasisi katika soko.  

Mkataba wao na Boateng unamaanisha mwanasoka huyo sasa anaweza kuonja soko la Marekani, Jay Z anaweza kuanza kujipanua kibiashara kwenye soka hasa upande wa Marekani na Bayern Munich nao watafaidika kwa kupata mtu ambaye anaweza kuisaidia timu kuongeza mashabiki ndani ya US. Wote wanaingia kwenyw biashara hii yenue hatari ndogo ya hasara.

Boateng anapata nafasi ya kufanya kazi na Jay-Z.

“Ni kweli nilifurahishwa sana kukutana na kubadilishana mawazo na Jay Z,” Boateng aliiambia BBC. “Jay Z ni mtu mzuri, mpole na mstaarabu na ana taarifa zote za kila
kinachoendelea.”

Nini kifuatacho?

Mpaka sasa, Roc Nation wamekuwa wakiandaa mazingira mazuri ya kusaini dili tofauti.
Wakati Kevin Durant alipokwenda barani ulaya kuuza viatu vya brand yake mwezi September, Boateng alikutana nae jijini Berlin, wote wawili wakajaribu kucheza michezo ya kila mtu baina yao na walipiga picha. 

Boateng amekuwa pia akipost material ya mtandao wa Tidal – mtandao mpya wa kusikiliza na kuangalia music wa Jay Z – pia amekuwa akiuhudhuria sana party mbalimbali huko LA.

“Sehemu ya kwanza ya mkataba wetu na Mwanaoka huyu ilikuwa ni kuijenga brand ya Jerome na kumuhusisha kimahusiano ya kikazi na kirafiki na mastaa wengine waliopo chini yetu,” anasema Yormark.

“Wakati tunapowaweka wanamichezo pamoja kama ilivyo kwa Kevin na Jerome, 1+1 ni sawa sawa na 3 kwa upande wetu.
“Pia tunawatambulisha wanamichezo wetu kwa wanamuziki wetu, kama Rihanna na Kanye west.
  
“Kwa namna anavyoendelea kutumia muda mwingi huku America, imani yetu ataweza kujitengenezea fursa.”

Sehemu ya pili ya dili lao – ni kusaini mikataba na makampuni – bado haijafikia muda wake.

“Kazi ilo jikoni na matangazo dili mpya kwake yatatolewa ndani ya siku 60 zijazo”. Je haitakuwa rahisi kaa Roc Nation kuwa- market aachezaji wanaocheza soka katika ligi ya Marekani?

Jibu linatoka kutoka kwa mmoja wa wateja wao.

Moja ya vitu vya kushangaza na vilivyovutia mwaka uliopita kwenye kombe la dunia ilikuwa ni Uchambuzi wa soka wa Rihanna kupitia akaunti yake ya Twitter – akitoa mitazamo yake kuhusu Luis Suarez, mbinu za Ujerumani na golikipa wa Argentina. Bado hajaonyesha kujua kiundani soka la America.

Mechi ya United States’ ya ufunguzi nchini Brazil katika kombe la dunia 2014 ilivutia watazamaji zaidi ya millioni 25 ndani ya US pekee – idadi kubwa zaidi fainali za NBA au baseball. Mwanzoni mwa msimu MLS, mechi zimekuwa zikivutia watazamaji wasiopungua 500,000.
“Sio lazima kwa Jerome kuja kucheza katika MLS ili aweze kuvutia fursa za kibiashara.” – alisema Yormark

“Jerome ni brand inayofahamika duniani. Mashabiki wa soka US wanaangalia soka la ulaya. Ikiwa atachagua kuichezea MLS baadae, itakuwa bora pia.” alimaliza Yormark.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here