Home Ligi EPL Je Emiliano Sala na rubani Wapo hai?

Je Emiliano Sala na rubani Wapo hai?

8336
0

Mambo bado yanaizid kuwa magumu kuhusiana na jibu la moja kwa moja kama Emiliano na rubani wake wapo hai ama lah. Inauma sana na inakatisha tamaa kwa siku 2 mfululizo jitahada za kujua angalau kama ndege ilidondoka ai ilitua.

Ukakasi umekuwa mkubwa, inakuwaje haionekani? Yaani wazungu na ujanja wao wote wamekwama? Hii ni hatari sana.

Kuna sauti inasamabaa mtandaoni ikisemekana kuwa ni Sala alipokuwa akiwasiliana na marafiki zake na baba yake.

“Hali ni mbaya hapa kwenye ndege. Inayumba sana na nahisi itadondoka. Naogopa sana. Kama itapita lisaa 1.5 bila kunisikia basi mjue hamuwezi kunipata tena.”

Maneno ya mwisho aliyotuma Emiliano Sala kwa marafiki zake

Kisha kuna sauti inasema “Baba naogopa sana, nisipokuwa hewani basi msitume mtu wa kunitafuta”

Hii inaashiria alikuwa katika wakati mgumu sana. Inasemakana hapo awali Ndege yao ilikuwa umbali wa hatua 5000s kwenda angapi, kisha baadae wakamweleza rubani ashuke mpaka umbali wa hatua 2000s. Baada ya kufika katika eneo hilo mawasiliano yakakata.


Hatma yake ni ipi?

Matumaini makubwa ya waogeleaji/wakoaji juu ya sakata la Emiliano Sala yamegawanyika katika pande 4.

1. Wametua nchi kavu lakini hakuna mawasiliano

2. Wametua majini wakabebwa na meli au chombo chochote cha majini lakini hawakuwa na mawasiliano

3. Wametua majini na kuondoka na vifaa maalum vya uokozi (maboya ambayo yalikuwepo kwenye Ndege)

4. Ndege ilipata ajali ikadondokea majini na kuwaacha wao wakielea*

Katika Matumaini yote hayo, waokoaji wanaamini zaidi katika tumaini namba 3 na wengi wao wameamia kutumia meli za uokozi katika maeneo yaliyotiliwa mashaka.

Rudi salama Sala

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here