Home Ligi EPL Je Cavani ataumaliza utawala wa Messi na Ronaldo kwenye tuzo za ufungaji?

Je Cavani ataumaliza utawala wa Messi na Ronaldo kwenye tuzo za ufungaji?

7452
0

Mpambano usioisha baina ya Lionel Messi vs Cristiano Ronaldo unategemewa kuendelea kwa muda zaidi.

Wawili hawa sasa wamelingana kwenye tuzo za Ufungaji bora baada ya Messi kushinda tuzo ya 4 Ijumaa iliyopita na kumfikia Ronaldo.

Hakuna mchezaji mwingine anayewasogelea katika ushindi wa tuzo hizo.

Swali liliopo sasa ni nani kati ya wachezaji hawa wawili ambaye atashinda tuzo ya 5 ya ufungaji bora? Mpaka sasa inaonekana shilingi imelalia upande wa Messi, Ronaldo mambo bado hayajamnyookea – amefunga magoli mawili tu katika ligi mpaka sasa, wakati Messi tayari amefunga magoli 12, ingawa bado yupo nyuma ya Ciro Immobile na Edinson Cavani wenye magoli 16.

Cavani ambaye anaunda utatu mtakatifu wa Paris Saint Germain na Mbappe na Neymar ndio anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ijayo ya ufungaji bora kwenye ligi za barani ulaya.

Katika misimu iliyopita, Cavani amekuwa akiangushwa na ukweli kwamba magoli ya Ligue 1 yana thamani ya point 1.5.

Ingawa msimu huu thamani iepanda mpaka kufikia pointi 2, sawa na ligi nyingine zikiwemo La Liga na EPL.

Msimu uliopita alifunga magoli 35 akiwa na PSG katika Ligue 1, Ronaldo ambaye hajashinda tuzo ya Golden Boot kwa miaka 2, alishinda tuzo hiyo msimu wa 2007/08 kwa kufunga magoli 31, msimu wa 2010/11 akafunga magoli 40, msimu wa 2013/14 akashinda kwa magoli 31 na msimu wa mwisho kuchukua 2014/15 akafunga magoli 48.

Last season, he scored 35 goals for PSG in Ligue 1.

Messi alitwaa tuzo hiyo msimu wa 2009/10 (34 goals), 2011/12 (50 goals), 2012/13 (46 goals) na 2016/17 (37 goals).

Wawili hawa walifikia level ya juu ya ufungaji ambayo ilionekana ni ngumu kuifikia muongo mmoja uliopita.

Messi alifunga magoli 50 na Ronaldo 48 – hii ndio misimu mizuri zaidi kwao kiufungaji – namba za kustaajabisha kabisa kwenye ufungaji wa magoli.

Lakini sasa kuna hisia kwamba wameanza kuondoka kwenye kilele cha ubora wao, huku Ronaldo akifunga magoli 25 msimu uliopita na mpaka sasa amefunga moja tu wakati ligi ikielekea katikati.

Hata hivyo bado kuna miezi mingi ya kubadili matokeo na huenda akarudi kwenye chati za ufungaji mpaka kufikia May 2018.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here