Home Ligi EPL Je Arsenal watavunja mwiko wa kutokushinda michezo miwili mfululizo ugenini

Je Arsenal watavunja mwiko wa kutokushinda michezo miwili mfululizo ugenini

41810
0

Arsenal mara yao ya mwisho kutia mguu St James’ Park walitandikwa mijeledi 2-1. Safari hii Unai Emery anawapeleka tena vijana wake kupimana ubabe na vijana wa Rafa Benitez siku ya kesho.

Washika mitutu hawa wa London (The Gunners) msimu huu wameruhusu mabao 8 kwenye mechi 4 za mwanzo. Mechi ya mwisho Arsenal wameshinda kwa tabu sana kwa Cardiff mabao 3 kwa 2. Kabla ya likizo fupi ya michezo ya kimataifa.

Newcastle takwimu zake zipoje?

Newcastle wameifunga Arsenal mara mbili tu katika michezo 23 ya mwisho ya mashindano yote (D5, L16). Emery nae anataka kuweka rekodi ya Arsenal kushinda mechi mbili mfululizo za ugenini tokea mwezi mei mwaka 2017.


Taarifa Arsenal


Alex Iwobi anarudi baada ya kuwa nje kwa majerha. Beki wa kushoto Sead Kolasinac na Ainsley Maitland-Niles nao wapo mbioni kurudi uwanjani baada ya kukumbwa na masahibu ya majeruhi.


Taarifa njema ni kwamba Laurent Koscielny ameanza mazoezi mepesi baada ya kuwa majeruhi kwa kipindi kirefu, huku Carl Jenkinson yeye bado anaendelea kupambana na majeraha yake ya kifundo cha mguu.


Arsenal wanaotumika adhabu?


Hakuna.


Mechi za Arsenal zifuatazo

Newcastle ugenini
Vorskla nyumbani
Everton ugenini
Brentford nyumbani
Watford nyumbani


Kikosi kinachotafajia kuanza

Emery hueanda akamrejesha Henrikh Mkhitaryan kikosini.
Baada ya Alexandre Lacazette kufunga bao moja na kitengeneza moja mchezo wao wa mwisho kuna uwezekano mkubwa akaanza mchezo huo.

Utabiri wa kikosi kwa mujibu wa jarida la goal.com

arsenal xi


Taarifa za Newcastle 


Nyota wa klabu hiyo Salomon Rondon na DeAndre Yedlin wanatarajia kuwemo kikosi licha ya uchovu wa michezo ya kimataifa. Taarifa mbaya kwa mashabiki wa Arsenal ni ujio wa Matt Ritchie na kiungo mkorofi Jonjo Shelvey ambaye ametokea kwenye majeraha.


Takwimu 

  • Mchezo wa mwisho Newcastle walishinda 2-1. Kama watashinda mchezo huo basi watakuwa wamerudia rekodi yao ya mwaka 1994 ambapo ilikuwa mara ya mwisho kuwafunga Arsneal mechi mbili mfululizo.

  • Mchezo wa mwisho Newcaslte ulivunja rekodi ya kufungwa na Arsenal mechi 10 mfululizo.
  • Newcastle ni timu ya 3 kufungwa na Arsenal mechi nyingi zaidi (26). Ya kwanza ni Everton (32) na West Ham United (29).
  • Mesut Ozil katika mechi 3 dhidi ha Newcastle amehusika mabao matatu (Mabao mawili, na asisti moja) Lakini hajawahi kukutana nao ndani ya St.James’ Park.

  • Tokea Newcaslte waifunge Arsenal mwezi April (2-1), Newcastle ilishinda mchezo mmojabtu kati ya 9 za Premier League (W1 D1 L7).
  • Fowadi wa Arsenal Alexandre Lacazette amehusika katika mabo 7 ya mwisho ya Premier League (5 mabao, 2 asisti).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here