Home Kimataifa Jadon Sancho hakamatiki

Jadon Sancho hakamatiki

3626
0

Jadon Sancho mzaliwa wa Camberwell nchini England. Amezaliwa 25 march 2000 na ana umri wa miaka 18 akitarajiwa kufunga miaka 19 mwezi wa Tatu mwaka huu. Kijana huyu sio mgeni masikioni mwa wapenda soka kwote Duniani kwani anacheza Borussia Dortmund na kwa mafanikio .

Safari ya Jadon ilianza katika klabu ya Watford mwaka 2007 alipo kaa katika kituo cha kukuzia vijana mpka mwaka 2015 ambapo klabu ya Manchester city ilimsajili. Amekaa katika klabu ya manchester city kwanzia mwaka 2015 mpka 2017.


Mwaka wa 2017 ndo ulikua mwaka wa Mafanikio kwa Jadon kwani ndio mwaka alioitwa katika kikosi kilichoenda kushiriki mashindano ya vijana wa chini ya miaka 17 wakiongozwa na Captain wa kikosi hicho Angel Gomez mchezaji wa Manchester united.

Katika mwaka huo walifanikiwa kuubeba ubingwa huo wa U-17 world cup. Hapa ndipo klabu yake ya sasa ilimuona na kumsajili na kumpa mkataba wa timu kubwaa. Jadon alicheza mechi yake ya kwanza ya klabu ya Borussia Dortmund tarehe 14 january 2018 ndipo safari ya kuchezea timu kubwa ilianza.


Msimu huu wa 2018 / 2019 umeonekana ni msimu wake wa mafanikio sana na hii ni baada yakua na muendelezo wa uchezaji mzuri na kuchagiza katika ushindi unaopatikana sana katika klabu ya Dortmund. Amekua na takwimu nzuri ambazo mpka sasa Anaongoza kwa Assist katika ligi hiyo ya bundasliga (9) pia amefunga magoli (6) mpaka sasa.

Kufuatia muendelezo wake mzuri katika klabu yake mwalimu South Gate alimuita mchezaji huyo kujumuika na kikosi cha wakubwa cha timu ya taifa na kumfanya kua mchezaji wa pekee anaetoka nje ya ligi ya England. Alicheza mechi yake ya kwanza katika mechi maalumu iliyokua ya kumuaga Wayne Roone aliingia kuchukua namba ya Sterling na katika mechi yake ya kwanza tuu alifanikiwa kutoa Assist.Umri wake haukuwa kizuizi kuaminiwa kutumikia klabu ya Dortmund kitu ambacho wenzake aliowaacha pale England wameendelea kuumia. Mfano wa wachezaji ambao ni rika yake ni Angle Gomez na Fil Foden ambao wote wamekua wakiitwa mara chache kuchezea timu za wakubwa.

Kama Borusia Dortmund wakibeba ubingwa mwaka huu basii mimi kwangu wachezaji hawa watatu sitaacha kuwataja katika mafanikio yao nao ni SANCHO, REUS , WITSEL.

@Sativa_clan

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here