Home Kimataifa Ivory Coast wakubali yaishe AFCON 2023

Ivory Coast wakubali yaishe AFCON 2023

3344
0

Ivory Coast imekubali kuandaa michuano ya mataifa ya Afrika 2023.

Hapo awali Ivory Coast ilikwenda mahakama ya michezo kuomba kutokuondolewa haki yao ya kuandaa 2021.

Raisi wa CAF Ahmad Ahmad alipeleka barua ya maombi kwa raisi wa Ivory Coast Alassane Ouattara. Raisi wa Ivory Coast alikubali maombi ya Raisi huyo wa CAF.

Mkutano hao ulihudhuriwa na waziri wa michezo wa Cameroon Paulin Danho, raisi wa soka wa Cameroon Sidy Diallo. Wajumbe wengine ni raisi wa FIF Sory Diabate, raisi wa kamati maendeleo ya soka masuala ya ndani ya soka wa Feh Kesse

Cameroon walichukua nafasi hiyo mara baada ya CAF kubadilisha ratiba ya hapo awali.

Ratiba ya hapo awali Cameroon walikuwa waandaaji wa mashindano ya mwaka huu kabla ya kuhamishiwa kule nchi Misri.

Guinea ambao walikuwa waandaji wa mwaka 2023 wataanda michuano hiyo mwaka 2025.


AFCON 2019 – Egypt
AFCON 2021 – Cameroon
AFCON 2023 – Ivory Coast
AFCON 2025 – Guinea

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here