Home Kitaifa Huyu ndiye Patrick Aussems

Huyu ndiye Patrick Aussems

5279
0

Wanamuita Patrick Winand J. Aussems. Alizaliwa tarehe 6 February 1965 katika kijiji cha Moelingen, Ubelgiji katika manispaa ya Voeren, sasa ni sehemu ni jimbo la Limburg. Alisifika kwa uchezaji wake wa nidhamu kama beki wa kati. Nafikiri hata sasa bado yupo katika misingi hiyo kinizamu. Japokua hakuna aliweza kumtazama enzi za uchezaji akiwa kijana lakini historia huwa haifichi.Akiwa na miaka tisa tuuh, alianza safari yake pale RCS Vise, klabu iliyo katika jimbo la Liege nchini Ubelgiji kuanzia 1974-81. Baadae akiwa kijana wa miaka 16 akajiunga na klabu Starndard de Liege hapa ndipo ulimwengu ulipo iona sura yake. Akiwa na umri wa miaka 18 na miezi 7, alicheza mechi yake ya kwanza katika ligi ya European Champions Clubs Cup sasa ni UEFA Champions league msimu wa 1982-83. Alicheza dhidi ya Athlone Town ya italia ambapo waliibuka na ushindi wa 3-2 wakiwa ugenini. Mechi ya marudiano walishinda 8-2. Na kutolewa hatua ya 16 bora na Dundee fc ya Scotland kwa idadi jumla ya mabao 4-0.Msimu uliofuata 1984-85 waliishiia hatua ya makundi kwa kufanikiwa kupata ushindi mmoja tuh! 3-2 dhidi ya FC tirol ya Austria. Wachezaji wenzake walijumuisha mlinda mlango mahiri Gilbert Bodart(mbelgiji), beki Michel Collard(mbelgiji), kiungo Zoran Jelikić (sebia), mshambuliaji Claudio De Oliveira (Brazil) na Alex Czerniatynski ambaye wabelgiji wanamkumbuka kwa kazi aliyoifanyia Starndard de Liege na taifa kwa ujumla.Hakuishia hapo tu, mwaka 1988-89 alijiunga na K.A.A. Gent ambapo alionyesha uwezo mkubwa, 1989-90 R.F.C Seraing na kwenda kumalizia uchezaji wake jiji la Troyes katika klabu ES Troyes AC mwaka 1990-92. Akiwa Troyes alianza kuwa kocha wa ES Troyes AC mwaka uliofuata baada ya kutundika daruga mpaka mwisho mwa msimu wa 1994-95. Alipo amia kufundisha SS Saint-Louisienne ya nchini Island kuanzia 1995-99. Baadae 1999-2001 alirejea Ufaransa, alifundisha klabu ya Capricorne Saint-Pierre. Na kufundisha vilabu vingine kama Stade Beaucairois na Stade de Reims vya nchini humo mpaka 2004.2005 alipata dili la kufundisha kadji sports academy ya Cameroon, 2005-06 karejea kwa mara nyingine Ufaransa na kufundisha SCO Angers. Baadae alipumzika mpaka 2009 Evian Thonon Gaillard F.C. ilipohitaji huduma yake, ndipo Shenzhen Ruby ya Uchina na Chengdu Blades ya china zilipata huduma yake kama kocha. Na 2013-15 AC Léopards Ya Demoklasia ya Congo, na baadae akapata dili kubwa la kuisuka timu ya taifa ya Nepal ambapo alifanya makubwa.Na sasa ni kocha mkuu wa Simba sports club, kwa kile alichokileta nchini Tanzania kina thamani kubwa, kufikisha klabu ya simba sports club katika hatua ya makundi ni jambo kubwa katika historia ya klabu hiyo, wahenga wanasema mwene nacho hungezewa. Na ukipata shikilia. Endapo klabu Simba sports club haitaleta uswahili tulio uzoea, naamini CAF champions league itakua ni jua, hata kuwe na mawingu vipi halijuiliwi kuchomoza. Na klabu itafika mbali.MWANDISHI : ISACK MSINJILI.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here