Home Kitaifa Huyu ndio Zana Coulibaly!

Huyu ndio Zana Coulibaly!

4403
0

Baada ya kuonesha kiwango kizuri na kuwashika mashabiki wa Simba, wakala wa Zana Coulibaly Faustino Mukandila amefunguka mambo kibao ikiwa ni pamoja na sababu za mchezaji wake kuanza kwa kusuasua alipojiunga na Simba.

KWA NINI ZANA ALIANZA KWA KIWANGO DUNI?

“Zana alikuja Simba akiwa hajafanya maandalizi ya pre season baada ya kuondoka Asec Mimosas. Zana ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kucheza nafasi zaidi ya moja na hujitoa 100% muda wote anapocheza.”

“Nadhani mashabiki sasa wameanza kumuona Zana mwenyewe japo hata watu ndani ya klabu hawakuwa na imani naye. Nafarijika kuona kijana anatoa mchango kwenye timu, anaipenda timu na mashabiki. Alibezwa sana na ilikuwa inaumiza lakini ukiwa mchezaji mzuri Mungu hakutupi wakati wowote.”

AMEWEZAJE KUREJEA KWENYE KIWANGO CHAKE LICHA YA KUZOMEWA NA MASHABIKI?

“Zana ni kijana anayejitambua, hata wakati alipobezwa alibaki kwenye malengo yake kwa sababu alikuwa anatambua muda wowote kiwango chake kitarejea. Hata sasa ambapo mambo yameanza kwenda sawa lakini bado hachukulii vitu poa. Mara kwa mara namkumbusha asimame kwenye malengo.”

ZANA ANAMAJUKUMU!!

“Anapendwa na mashabiki lakini kijana mwenye mke na mtoto ambao wanamfanya kuwa kijana mwenye majukumu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here