Home Kitaifa Hongera sana Jokate lakini usiwasahau akina Hazard

Hongera sana Jokate lakini usiwasahau akina Hazard

12297
0

“Unyenyekevu, busara na hekima nijalie eh Mungu Wangu” Jokate Mwegelo.

Nataka niwahadithie kitu. Hapo zamani palikiwepo na wakulima walisemekana walikuwa wamelala shambani nchini fulani. Wafanyakazi wengine wakalalamika wakasema “HAWAFAI” wakaja juu kwa mihemko “HATUTAKI TENA WAKULIMA WAZEE”

Akaja bwana shamba mmoja. Watu wakumuomba bwana shamba asiajiri tena WAZEE. Yule Bwana Shamba akateua mwanadada mdogo mdogo tu hivi umri wa miaka 25-35. Wale wafanyakazi wakaja juu tena “HATUTAKI VIJANA WADOGO HAWAFAI” hadithi yangu imeishia hapo.

Nikwambie kitu ndugu yangu unayesoma makala hii. Haijalishi una wakati gani. Hivi majuzi Ali Kabla ya Ali Kiba kuoa watu walimzonga sana Jokate kutemwa kwenye uongozi wa chama chake. Sisi hatujui kilichotokea ila mitandaoni watu walimchafua sana.

Baadae kidogo Ali Kiba akaoa. Kuna taarifa zikidai alikuwa mchumba wake hapo awali (Mimi sijui na sifahamu nimesikia) Watu wakamvamia Jokate mitandao kwa kebehi kejeli na kila aina ya neno chafu.

Hapo alitukanwa au kukejeliwa na wale waliomsema kutokana na uongozi jumlisha wale waliomzomea kwa sababu ya ndoa ya Ali Kiba. Bila shaka hata ni ni wewe ungekuwa kwenye fedheha.

Nahisi huyu dada alipita kipindi kigumu sana kwenye mitandao. Lakini amini Mungu yypo. Unapokuwa chini huwa anataka kuwaonesha maadui zako kuwa wewe una ujasiri wakuvumilia shida na una nguvu ya kusimama tena.

Nimefurahi hii leo kuona video ya Ali Kiba akihojiwa na kituo cha Millard Ayo. Aliulizwa kuhusu Jokate yeye ana ujumbe gani kwake hasa baada ya kuteuliwa.

“siwezi kuongelea chochote kuhusu Jokate” Hapa alisita sana lakini alipogundua umuhimu wa nafasi aliyopata Jokate akaendelea kusema “Kiukweli kifupi (kwa msisitizo zaidi akaweka mpaka neno la kiingereza “Inshort) nimefurahi na nampa hongera” Fulustopu. Mwanzoni alisita kidogo kwa sababu hakuelewa mantiki ya swali lakini chuki yeyote Ali Kiba huyu huyu ambaye sie tumemweka kwenye kundi la uadui na Jokate (ingawa sijui kama ni marafiki au maadui kwa sasa)

Kwanini nampomgeza Jokate?

Jokate ni mdada mwemye moyo wa kipekee kwa kumuona na kwa kumsikia mimi simjui zaidi ya hapo (Nisije nikawa mnafiki). Lakini kuna tukio moja nalikumbuka kwake ambalo linanifanya nitumie muda wangu kumuongelea.

April 8, 2018 Shaffi Dauda na Jokate waliongozana mpaka ilala bungoni kwenda kukutana na kijana Hazard. Kupitia Jokate Shaffih akakubali kumjumuisha Hazard kwenye kampuni yake ya Shadaka Sports Management.

Hazard ni nani? Anafahamiana vipi na Jokate?

Mwaka juzi Jokate alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondari Majani ya Chai, Hazard alitangazwa mwanamichezo bora hivyo akakabidhiwa zawadi (tuzo) yake na Jokate.

Baada ya muda akaanza harakati za kumtafuta Jokate ili kumweleza juu ya kipaji chake na kuomba msaada asaidiwe kufikia malengo. Hakuwa na namba ya simu wala hakujua atakutana wapi tena Jokate hivyo haikuwa kazi rahisi kwake, ndipo alipoamua kutmia mtandao wa Instagram kufikisha ujumbe wake.

Alikuwa akimtumia ujumbe kupitia DM (Ujumbe Instagram) lakini kutokana na harakati na majumu mengi Jokat hakuwahi kuzisoma. Hazard hakukata tamaa kwa sababu aliamini ipo siku. Akamtumia picha zake akiwa mazoezini na kumkumbusha anahitaji yake.

Machi 20 ya kila mwaka Jokate Mwegelo huadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (birthday), Machi 20 mwaka huu (2018) Hazard alipost picha ambayo alikuwa akipokea tuzo ya mchezaji bora aliyokabidhiwa na Jokate miaka miwili liyopita kisha akam-tag Jokate. Kama haitoshi akamtumia Jokate picha hiyo DM na kumkumbusha historia ya picha hiyo.

Katika peruziperuzi za Jokate kwenye simu yake akakumbana na sms na picha za Hazard, zilikuwa nyingi na zinaelezea lengo lake la kutaka kufika mbali katika nia yake ya soka. Jambo jema ni kwamba katika jumbe ambazo Hazard alikuwa amemtumia Jokate aliwahi kutuma na namba yake ya simu ya mkononi kwa hiyo Jokate alimpigia simu wakazungumza mengi na kumuahidi atakwenda nyumbani kwao kumtembelea na kuona namna ya kumsaidia.

Nimemaliza simulizi yangu (Asante bwana dick kwa simulizi hizi, ukitaka kusoma makala nzima ya Jokate na Hazare Click Hapa).

Jokate wakati huo hakuwa kiongozi yeyote. Alikuwa tu mtu kama mimi ingawa anapicha kubwa ndani ya jamii.

Jokate ni mwanamichezo mzuri. Ni mwanamitindo. Leo hii ameonesha nia ya dhati kumsaidia kijana mdogo kama yule je leo akiwa Mkuu wa Wilaya atasaidia wangapi? Je kesho akiwa mbunge? Vipi keshokutwa akiwa waziri? Mtondo go akiwa waziri mkuu?

Hii ni moja fursa kubwa kwetu sisi wapenda michezo. Tumepewa kijana mwenzetu. Nawashangaa mazezeta ambao mwanzoni waliponda uwepo wa wazee kwenye vyeo mbalimbali kisha leo wanaponda kijana mwenzao kupewa cheo? Kwanini tusimpongeze Jokate na kumpa moyo? Au mlitaka nyie ndio mpewe hicho cheo? Mbona raisi wa Croatia alikuwa mwanamitindo? George Weah alikuwa mwanasoka na leo ni Rais kwanini iwe kesi kwa mwanamitindo? Mna matongotongo rudini mkanawe.

Aliyekwambia kijana akipewa cheo atawaza uhuni ni nani? Vipi akina Januari Makamba si vijana wadogo? Na kwanini mnamhukumu Jokate katika uga wa uhuni? Nani aliyewambia kila mwanamitndo ni mhuni? uhuni sio umakamo ila ni hulka ya mtu.

Jokate baada ya kupata cheo amemuomba Mungu unyenyekevu wa kuongoza.

“Unyenyekevu, busara na hekima nijalie eh Mungu Wangu”

Kama ulivyoomba dada Jokate naamini atasikia ombi lako.

Hongera Jokate sikufahamu ila hata mimi ningetamani kufanya kazi Kisarawe Si Unajua hata mimi darasa la 7 nilipewa tuzo ya mwanamichezo bora ila sasa huyo aliyenipa hiyo tuzo daah…(Natania).

Samahani Mheshimiwa Jokate huko juu nimeandika jina lako bila kuweka neno Mheshimiwa.

Hapa ni website ya shaffihdauda pia tupo Instagram na facebook kwa jina hilo hilo. Usisahau kuingia dauda tv youtube uoate habari za uhakika.

Mimi naitwa Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here