Home Ligi EPL Historia fupi ya klabu ya Yanga

Historia fupi ya klabu ya Yanga

4840
0

Klabu ya Yanga ni moja ya vilabu vikubwa sana hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Ina mafanikio nje na ndani ya Tanzania. Siku ya leo klabu hii kubwa na yenye historia ndefu imetimiza miaka 84 sasa.

Makala na Priva Abiud (Privaldinho)

Miamba hii ya Jangwa ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1935. Hapo baadae kwenye mwaka 1936 klabu hiyo ikavunjika baada ya wajumbe wa kamati ya klabu kushindwa kuelewana.

Wajumbe hao wakakubaliana kugawanya klabu hiyo na kuanzishwa klabu nyingine. Klabu iliyojiengua ilijulikana kama Queens FC ambapo baadae walijiita tena Eagles. Klabu hiyo ya Eagles ilibadilishwa tena jina na kujiita Dar Sunderland.

Ilipofika mwaka 1michuano hii ambapo pia walifika971 wakjipatia jina jipya ambalo kwa sasa ni moja ya majina ya kutisha kwenye historia ya soka la Tanzani Simba Sports Club unaweza pia kuwaita Wekundu wa Msimbazi au mnyamaa

MAFANIKIO
Yanga hii yenye historia kubwa na ya kuvutia hapa nchini imefanikiwa kutwaa mataji 27 ya ligi kuu. Kwa heshima kubwa waliyonayo wana jangwani bila kupepesa unaweza kuwaitwa mabingwa wa kihistoria.

Makombe ya ligi bado hayakuwatosha, nje ya mipaka ya nchin walinyakua tena vikombe kadhaa ikiwemo kombe la CECAFA mara 5 na matajai mengi lukuki ndani na nje ya taifa.

Klabu hii iliyotukuka kwa mafanikio kem kem ndani ya taifa hili haipo nyuma pia kwenye michuano ya kimataifa. Katika michuano ya klabu bingwa afrika ilishiriki kwa mara ya kwanza mwaka 1969 ambapo ilifanikiwa kuonja utamu wa michuano hiyo mikubwa kunako bara la Afrika kwa kutinga hadi hatua ya robo fainali.

Kutokana na utamu ule Mwaka uliofuata 1970 vidume hawa wa jangwa wakajaribu tena kuchovya tena kwenye michuano hii ambapo pia walifika hatua ya robo fainali.

Yanga wakijiita Young Africans hata kwenye kombe la shirikisho imefanikiwa kuingia hatua ya makundi mara mbili, 2016 na 2018.

Kule kunako Kombe la washindi la Afrika pia wanajangwani walifika hatua ya robo fainali mwaka 1995. Bila shaka Yanga ni moja ya urithi wa kisoka tunaojivunia watanzania kwa mafanikio yake yaliyotukuka ndani ya taifa hili.

Mmoja kati ya wachezaji wenye heshima kubwa katika soka waliowahi kucheza Yanga ni Shaban Nonda raia wa Burundi aliyechezea klabu hiyo miaka ya 1994 kabla ya kwenda Afrika Kusini, kisha akajiunga na FC Zurich, Rennes na Monaco za Ufaransa, Roma ya Italia, Blackburn Rovers ya England, pamoja na Galatasaray ya Uturuki.

Wachezaji wengine wa ndani ni kama Sunday Manara Kompyuta ambaye pia aliwahi kucheza nje ya nchi, Marehemu Maulid Dilunga na mlinda lango Elias Michael.

Heri ya kuzaliwa wanajangwani Asanteni kwa mafanikio kiduchu mliyopata kimataifa ingawa hapa kwetu na kwenu ni heshima kubwa kwa sababu hakuna aliyekuzidi sana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here