Home Kitaifa Hii Simba hii haponi mtu taifa

Hii Simba hii haponi mtu taifa

4810
0

Napenda kuwapa pongezi kubwa Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Simba, kwa kuanza kampeni zao za hatua ya makundi kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura, ya nchini Algeria.

Mchezo ulikuwa wa kuvitia sana kwa pande zote mbili Algeria, walianza kwa presha kubwa sana huku wakiamini wataweza kuivuruga mipango ya Simba.

Simba walijaribu kuwasoma wapinzani wao jinsi wanavocheza ukiangalia katika idara ya Kiungo Simba, muda mwingi walitawala mchezo uwiano wa ule utatu wa hapo kati ulikuwa umeleta mafaa sana ukimuangalia Kotei, Mkude, na Chama, kila mchezaji alikuwa anafanya jukumu lake.


Historia ya Simba hatua ya makundi
Mechi 7
Magoli ya kufunga 10
Magoli ya kufungwa 10
Clean sheets 3


Eneo la Kiungo mkabaji muda mwingi Kotei alikuwa akicheza chini sana kuwalinda mabeki huku wakiamini Js Saoura, ni wazuri kwenye kushambulia kwa mpira ya kushtukiza kutoka nyuma kwenda mbele Mkude, alikuwa anafanya kazi moja kuchukua mpira na kumpa Chama, kupandisha mashambulizi nidhamu ya mchezo kwa Simba, ilikuwa ipo juu sana walikuwa wanacheza kwa tahadhari sana.Katika idara ya safu ya ulinzi watu wengi baada ya kuumia Erasto Nyoni, wengi waliamini kulikuwa hakuna beki wenye uwezo Kama wake au mwenye uzoefu na mechi za kimataifa ukimtoa Pascal Wawa,

Juko alipewa nafasi lakini muda mwingi alikuwa ajiamini sana pengine huwa achezi mara kwa mara muda mwingi Pascal Wawa, alikuwa ana sahihisha makosa yake kipindi cha pili alicheza vizuri mno sisemi kama ataweza kuziba pengo la Nyoni hapana? bali anaweza kufanya kile kitu ambacho mwalimu amemuagiza.


Simba imefikisha idadi ya magoli 89 kwa klabu bingwa


Katika eneo la ushambuliaji Okwi, leo ndo mwiba wa JS Saoura, muda mwingi alikuwa akizunguka uwanjani kutafuta mpira Kwanza ana uwezo wa kukaa na mpira kupiga chenga muda mwingi alikuwa akiwafanya mabeki wa timu pinzani wasipande kushambulia.

JS Saoura, walitegemea wacheze kwa kujilinda na kutengeneza nafasi za kufunga utatengenezaje nafasi? Ukiwa mbele umewaacha wachezaji wawili au moja?

Ile kauli ya msemaji wa klabu ya Simba Yes we can imetimia mungu ibariki Tanzania mungu ibariki Afrika.

Azizi Mtambo 15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here