Home Kimataifa Higuain In, Morata Out

Higuain In, Morata Out

4595
0

Taarifa za kuaminika zinadai kuwa klabu ya Atletico Madrid ipo mbioni kumnasa nyota wa Zamani wa Madrid na Juventus ambaye kwa sasa anakipiga kunako klabu ya Chelsea Alvaro Morata.

Baada ya kuwa na msimu wenye milima na mabonde, Morata anataraji kurudi tena nyumbani kwao. Zamu hii sasa anakwenda kwa Mahasimu wa klabu yake ya zamani Atletico Madrid.

Taarifa zinaeleza kuwa Morata atajiunga kwa mkopo Atletico wa mwaka mmoja na hapo baadae klabu hiyo inaweza kumnunua moja kwa moja.

Morata atafuata nyayo za Diego Ciasta ambaye pia aliwahi kuichezea Chelsea kabla ya kurudi tena Atletico. Hapo awali aliyekuwa nyota wa zamanibwa Liverpool na timu ya taifa ya Hispania, Fernando Tores nae mambo yalimwendea kombo pale darajani kabla hajatimka.

Tores pia baadae nae aliamua kujiunga na Atletico akitokea nchini Italia. Msimu uliopita Morata alikosa nafasi za wazi 27 akiwa mchezaji namba 2 aliyekosa nafasi nyingi nyuma ya Mo Sala (35) . Licha ya Mo Salah kukosa nafasi nyingi alifunga mabao 44 lakini Alvaro alifunga magoli 16 pekee


Kule nchini Italia nako, taarifa zinasema muda wowote Higuain atatua darajani kwa mkopo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here