Home Ligi EPL Hela zinawatoa povu Klopp na Mourinho

Hela zinawatoa povu Klopp na Mourinho

9816
0

Mourinho, ameeleza kwamba kocha mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp anapaswa kushinda kombe msimu kutokana na usajili mkubwa aliofanya. amesema hayo baada ya Liverpool kutumia zakdi ya £185m katika wiki kadhaa zilizopita.

Mourinho pia amemtahadharisha Klopp kuhusu matumizi makubwa ya fedha kwenye usajili. Kauli ya Mourino ni kama kebehi kwa Klopp ambaye aliwahi pia kumsema Mourinho vibaya kutokana na matumizi yake makubwa ya usajili.

Klopp amesema kauli ya Mourinho ni ya majungu na yana chembe za unafiki ndani yake

Klopp alipoulizwa kuhusu kauli ya Mourinho alisema anachezea akili za watu. Hakuna jambo la maama kabisa ila anajaribu kuwapotezea watu umakini wao katika kazi.

“Nimesikia Jose ametumia kauli ya utani kwangu baada ya kusikia tumetumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye usajili. Moja ya malengo yangu makubwa ni kumfanya mourinho atabasamu. Haitokeagi sana lakini kwakuwa nimefamya hivyo nikiwa na Liverpool ni jambo jema”

“Najua nimewahi kusema mambo mengi hapo awali ila sikumbuki yote ila nachokumbuka niliwahi kuongelea usajili wa Pogba”

[Siku kwenye maisha yangu ikitokea nimemnunua mchezahi kwa gharama kama za Pogba sitokuwa kocha wa soka wakati huo. Hii ilikuwa kauli ya Klopp aliyotamka baada ya United kutoa £89m kumnunua Paul Pogba mwaka 2016]

“Siwezi kuongelea kuhusu Man United labda ikitokea mtu ameniuliza. Lakini mimi ni mpole sana kutoa majibu ikiwa mtu ameniuliza kuhusu hiyo timu.

“Sio rahisi hata kidogo kuizungumzia Man United. Lakini pia sina tatizo na Jose Mourinho. Najua anaongea sana. Siwezi kumzuia maana hii ni dunia huru. Mtu anaweza kuongea anachojiskia.

“Nimefurahi kuona ameongelea usajili wetu. Lakini nachokijua usajili mkubwa haukupi nafasi ya moja kwa moja kutwaa ubingwa.

“Man United imekamilika kila idara na nadhani wiki mbili zijazo wataongeza nguvu mpya, Man City ni timu hatari na Tottenham wapo vizuri hivyo huwezi kusema eti msimu lazima nibebe ubingwa”

“Arsenal na Chelsea wamepata makocha wapya, nina imani pia wao wana malengo yao makubwa maana kila mmoja ana mipango yake na timu zao pia zina vikosi vizuri. Hivyo ni wajibu wetu kutengeneza timu imara na huwezi kufanya hivyo kirahisi maana masokoni mambo hayafai bei za wachezaji zimefumuka sana”

“Kufanya marekebsisho katika kikosi sio kununua tu wachezaji ila pia kucheza vizuri, kutafuta matokeo kwa bidii na kufurahisha mashabiki wanaokuja uwanjani. Sisi ni Liverpool na tutajitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu tuone tutafika wapi”

Usajili mpya wa Liverpool wa mlinda lango Alisson unaiwekea Liverpool rekodi kubwa ya usajilo dhidi ya Man United tokea mwaka 2016 kufikia kiasi £411.55m, ukilinganisha na United kiasi cha £392.55. Kumbuka United haikulipa ada yeyote kwa kwa Alexis Sanchez na Zlatan Ibrahimovic.

Liverpool ina beki ghali zaidi van Dijk, £75m kutoka Southampton, huku united ikiwa na kiungo ghali zaidi duniani Paul Pogba, Juventus £93.25m. Liverpool pia ikiwa na kipa ghali zaidi duniani.

Huenda Mourinho akavunja rekodi hii ya Liverpool kama watafanya usajili wiki mbili zijazo.

United imepokea kiasi cha £85.3m kama ada za uhamisho tokea Mourinho ajiunge na mashetani wekundum Memphis Depay £21.7m ikiwa dau kubwa zaidi, lakini Liverpool wakipokea £289.65m bila kusahau dau nono la £146m kutoka kwa Barcelona kwenye usajili wa Philippe Coutinho.

Mourinho na United wanaonekana wao kumia zaido hela nyingi ukilinganisha na Klopp wa Liverpool

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here