Home Kitaifa Heeh! Kumbe Masoud Kipanya aliacha soka kisa KATUNI!

Heeh! Kumbe Masoud Kipanya aliacha soka kisa KATUNI!

3710
0

Ebwana mkali wa kuchora cartoons Masoud Kipanya ‘KP’ inawezekana kabisa kama isingekuwa issue za uchoraji basi pengine angekuwa bonge la mchezaji wa enzi hizo kwa sababu anasema akiwa mdogo alikuwa anapiga sana ‘chandimu’.

Baadaye akapiga chini soka kwa kuogopa kuvunjika mkono ambao tayari ulikuwa unamuingizia mkwanja kutokana na kazi zake za uchoraji.

“Niliwahi kucheza mpira lakini ule wa makaratasi (chandimu), lakini nilianza kuchora nikiwa mdogo sana na ilikuwa inanilipa nikiwa mdogo kwa hiyo nilivyokuwa nikiingia uwanjani nilikuwa naogopa sana nisipate madhara kwenye mkono (anaoutumia kuchorea) kwa sababu mpirani kuvunjika ni kitu cha kawaida”-Masoud Kipanya.

“Mpira tuliokuwa tunacheza wakati ule jioni au shuleni ilikuwa bado hatujafikia kulipwa, lakini mkono wangu tayari ulikuwa unanilipa kwa hiyo nilijikuta naogopa sana kucheza nikajikuta naachana na mpira.”

Aisee noma sana, kuna watu wameanza kutengeneza CASH tangu wakiwa makinda👐 wewe umeanza kulipwa lini kutokana na kazi yako?

#Source: Nyundo ya Baruan Muhuza #AzamTV

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here