Home DOKUMENTARI Guardiola na Zlatan Nusura wazichape

Guardiola na Zlatan Nusura wazichape

9571
0

Simulizi ya Maisha ya Zlatan

Hii Sehemu ya 9

Hatimaye maisha yake Inter Milan yalifika ukomo. aliamua kuondoka zake. Alipotua Barcelona alikwenda kutimiza ndoto zake ambazo alikuwa nazo tokea akiwa Sweden. Shida kubwa ndani ya Barcelona ilikuwa Lionel Messi  na Pep Guardiola. Ibra anasema katika maisha yake Barcelona kisiki kikubwa ilikuwa ni kutwaa nafasi ya Messi pale Camp Nou. Shida kubwa ya aliyoiona kwa Messi alikuwa kama mtoto wa mama.

Messi akiwa na Zlatan

Nilianza msimu vizuri lakini alianza kulalamika kuhusu aina yangu ya uchezaji. Alisema kuwa hataki kucheza kushoto na Guardiola alimwelekeza kucheza namba 9. Nilijua wazi yale yalikuwa mawazo ya kaka yake (Guariola) maana walikuwa wanapenda sana na muda mwingi walikuwa mazoezini wanaongea wao wawili.

Messi na Guardiola Mazoezini

Messi wakati nakwenda alikuwa Winga. Guardiola alipenda kutumia mfumo ulikuwa 4-3-3 lakini kwakuwa Messi alilalamika ukabadlishwa na kuwa 4 5 1. Mfumo huu uliniyima amani kwani nilikosa uhuru uwanjani.

Pale Barcelona nilijitahidi sana kuwa kama mtoto mdogo ili nifanane na hao watoto wao la Masia. Nilijifanya kama mwanafunzi. Kila mtu aliniambia maisha ya pale ni magumu sana. waliniambia sipaswi kutumia ndge binafasi. Nilikuwa nasafiri kwenye ndege za abiria wengine. Yaani kila safari tulipanda ndege moja tu.

Nilishangaa sana maisha ya Guardiola.

Mpira wakawa wanacheza wao tu. Nilisajiliwa kama mchezaji mkubwa na kwa heshima hiyo nilitaka kuleta mafanikio ndani ya klabu. Siku moja tuligombana mazoezini, mchezo uliofuata alinichezesha dakika tano dhidi ya Villareal. Alikuwa mwepesi wa kumwekea mtu kinyongo.

1981:  Alizaliwa October 3 – Mjini Malmo.
1996: Akasajiliwa na Malmo FF, akiwa na miaka 15.
2000: Alikataa kujiunga Arsenal.
2001: Akajiunga Ajax kwa rekodi ya Mswedish wa gharama kubwa zaidi £7.7million.
2004: Akajiunga Juventus kwa £14m akafunga 16 msimu wa kwanza
2006: Akatimkia Juventus £21m.
2009:  Akajiunga Barcelona kwa £39m +Samuel Eto’o.

Kila mara alikuwa ananifuatilia kama mchawi, na hii ilinifanya nikose uhuru klabuni kabisa. Baada ya kutolewa na Inter Milan kwenye michuano ya UEFA, Guardiola aliingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na alikuwa akinitazama mimi utadhani mimi ndiye sababu ya sisi kufungwa.

Niliamua kumfokea nikamwambia nitapasua hicho kipara kwanini unaniangalia vibaya?. Pep alichukia sana. Alitaka kunisogolea nikwambia asije akathubutu, maana nitamvunja vunja wala sitojali kabisa. Nikamfokea sana kila mchezaji alikaa kimya, kila mtu klabuni aliniogopa kwa sababu sikuwa na masikhara. Maxwell pekee ndiye mtu niliyelewana nae.

Nikamwambia Pep kuwa “najua unachukiana sana na Mourinho na hiyo chuki itakuua.

Nilibadilika nikawa chizi ghafla, pembeni  yangu palikuwepo na boksi la vifaa vya mazoezi nikalipiga teke kwa hasira, Nikaparaza sakafu makusudi nikaiharibu marumaru yake. Guardiola aaogopa tu wala hakuniambia chochote akaamua kurudisha vile vifaa kwenye boksi na akaondoka zake” alisema Zlatani.

Alikuwa anamchkia sana Mourinho kwa sababu alijua kuwa yeye pekee ndiye mpinzani wake mkubwa

Guardiola alijenga timu chini ya Xavi, Iniesta na Messi. Zlatan alitumika kama mchezaji wa pembeni nafasi ambayo ilikuwa ngumu kwake kufanya vyema. Zlatan anasema Guardiola aliongea kihispaniola akimwambia Xavi na Iniesta kuwa kila mpira wampe Messi. Walidhani sielewi lakini nilikuwa nafahamu kila kitu.

Huwezi kununua Ferrari kasha uendeshe kama Fiat. Kwanini walininunua kama walikuwa wanahitaji mchezaji tofauti na mimi.

Nikiwa Ajax, Barcelona niliona kama klabu kubwa sana duniani. Na niliamini hivyo. Na ndivyo ilivyokuwa. Lakini nilipofika klabuni pale hakuna mchezaji hata mmoja aliyekuwa akiishia kama supasta. Walikuwa washambawashamba sana. Yaani utadhani ni watoto wa shule. Kwanza walituambia hupaswi kuja na gari la kifahari mazoezini. Siku moja nilifika na gari yangu ya mazoezi nikapaki mbali kidogo na uwanja wa mazoezi.

Mzigo wake huu unaitwa Porsche 918 Spider. bei yake ni US$845,000

Nilipofika Guardiola akaniambia umevunja sheria za hapa.

Nikamuuliza zipi akasema huruhusiwi kuja na gari ya kifahari. Nikamwambia siwezi kupanda teksi na sina gari ya bei ndogo.

Mafanikio ya Guardiola kama Kocha

Barcelona

La Liga: 2008–09, 2009–10, 2010–11
Copa del Rey: 2008–09, 2011–12
Supercopa de España: 2009, 2010, 2011
UEFA Champions League: 2008–09, 2010–11
UEFA Super Cup: 2009, 2011
FIFA Club World Cup: 2009, 2011

Kesho yake nikabeba Ferrari yangu mpya (enzo) makusudi na niakenda nikapaki karibu na mlango wa kuingia uwanjani nikaziba kabisa mlango nikaacha upenyo wa mtu kupita. Walinzi walitamani kuniuliza lakini waliogopa.

Baada ya tukio lile alikuwa hanitazami kabisa usoni. Alikuwa na kiburi na anasusa kama mtoto wa kike. mimi ni penzi cha magari ya kifahari leo mtu ananiambia nisitembelee magari hayo? kama ana roho ya kimasikini kwanini anataka anirithishe na mimi?

Messi, Xavi na Iniesta ni wachezaji waliokuwa na vipaji haswa lakini kila saa wanatembea wameinama yaani wapo wapo tu utadhani sio mastaa kabisa. Hawajui hadhi yao ulimwenguni ni ipi. Walikuwa washamba wa mambo mengi sana.

ZLATAN IBRAHIMOVIC KWENYE LA LIGA 2009-10

Period Michezo G Assisti kadi Nyekundu
 31 Aug-12 Dec 14 11 5 4 0
16 Dec-16 May 16 5 3 2 1

 

kitu cha Volvo

Kwenye kitabu chake Ibra ansema kuwa “kocha mzuri ni Yule ambaye hasusi ovyo, makocha wakubwa hata kama anaweza kuongea na wachezaji 20 kitokea wa 21 haongei nae lazima ahakikishe ajue shida ni nini. Mchezaji mmoja anaweza akaharibu mudi ya wale wengine 20 na ukawapoteza wote. Wengi wanamsifia sana Guardiola kuwa alibeba makombe 6. Msimu ule hata mimi ningekuwa kocha ningetwaa makombe yale.

                                                MAWAZO YANGU

 

Kila mtu alishangazwa kwa namna Ibra alivyokuwa akichukuliwa Barcelona. usajili wake ulionekana kama wa Presha na chuki dhidi ya Eto’o na kwa hili dili lao waliiumbuka sana. Msimu wa Mwisho Eto’o alifunga magoli 36 lakini Pep aliona bado kuna kasoro licha ya kutwaa vikombe vitatu. Msimu wa kwanza wa Zlatan Klabu ilitoa Milion 75 kumpata lakini waliishia kutwaa kikombe kimoja.
BARCELONA 25/10/09.-  Zlatan Ibrahimovic ( Carles Puyol (), Leo Messi (), Sergi Busquets Gerard Piqué

Kwa kikosi kile walikuwa na uwezo wa kubeba makombe bila hata ya kocha. Makocha wadogo wadogo ndo wenye tabia ya vinyongo. Guardiola anavyoongea kwanza ni mnafiki sana. Anapenda kuonekana mbele ya watu kuwa ni mwema. Ni sawa na Tiger Woods tu. Barcelona ilikuwa kama watoto wa shule, mimi tu nilikuwa wa tofauti maana kila mara niliuliza maswali kuhusu mbinu za mwalimu.

Ibra alipoona kiwango chake kitaoza alituma barua ya kuomba kuuzwa.
Lakini Pep Guardiola alitaka kuficha ficha mambo kwa kudai kuwa Zlatan haondoki. 
Zlatan akatamka hadharani kuwa kama hatomruhusu kuhama.

je wataka kujua Zlatan alitamaka nini? naam… basi tukutane makala ijayao.. Imeeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here