Home Kimataifa Guardiola kwenye mtihani mwingine

Guardiola kwenye mtihani mwingine

3130
0

Everton Vs Manchester City, mchezo huu utapigwa katika dimba la Goodson Park, leo Jumatano, majira ya saa 22:45 usiku.
.
.
Everton, wameshinda mchezo moja kati ya michezo 11 ya mwisho kwenye ligi kuu England dhidi ya Manchester City, sare 4 na amepoteza mara 6 mara ya mwisho Everton, kumfunga Manchester City, ilikuwa mnamo mwezi January mwaka 2017 kwa mabao 4-0 katika dimba la Goodson Park.
.
.
Manchester City, wameshinda michezo miwili kati ya michezo mitatu ya mwisho kwenye ligi kuu ya Ugenini dhidi ya Everton, amepoteza mara 1 pia katika michezo 17 ya mwisho kwenye dimba la Goodson Park, kwenye michuano yote City, ameshinda mara 2 sare 5 na amepoteza mara 10.
.
.
Manchester City, wanaangalia uwezekano wa kushinda michezo miwili mfululizo dhidi ya Everton, kwa mara ya Kwanza mara ya mwisho ilikuwa msimu wa mwaka 2013-14 wakiwa na kocha Manuel Pellegrini.
.
.
Everton, wamepoteza michezo mitatu kati ya michezo minne ya mwisho kwenye ligi kuu katika uwanja wa nyumbani ameshinda mara 1 pia katika michezo 23 waliyocheza katika uwanja wa nyumbani ameshinda mara 13 sare 7 na amepoteza mara 3.
.
.
Manchester City, wamepoteza michezo mitatu kati ya michezo mitano kwenye ligi kuu katika viwanja vya ugenini ameshinda mara 2 pia katika michezo 34 ya ugenini ameshinda mara 26 sare 6 kupoteza 2.
.
.
Pep Guardiola, ameshinda michezo yote minne kwenye ligi kuu England aliyokutana na kocha wa Everton, Marco Silva, kwa jumla ya mabao 15-3.
.
.
Theo Walcott, amefunga mabao matano kwenye ligi kuu England dhidi ya City, pia Westham, ndo timu aliyoifunga mabao mengi mabao sita Wallcot, mabao matano amefunga katika michezo saba dhidi ya City.
.
.
Sergio Aguero, amefunga katika michezo minne ya City, kwenye michuano yote amefunga mabao sita katika mashuti nane yaliyolenga golini katika dakika 360.
.
.
@Azizi _Mtambo _15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here