Home Ligi EPL Guardiola arusha kijembe cha chini chini kwa Man United kwa matumizi ya...

Guardiola arusha kijembe cha chini chini kwa Man United kwa matumizi ya mipira mirefu

585
0

1Pep Guardiola ameendelea kuwachimba Manchester United chini chini kwa matumizi yao makubwa ya mipira ya mirefu na kudadavua anachopenda hasa kifanyike kwenye timu yake.

Guardiola leo atakuwa na kibarua kigumu mbele ya West Brom kwenye dimba la Hawthorns, mchezo ambao utakuwa mgumu kwake kufuatia kucheza michezo sita mfululizo bila ushindi, rekodi ambayo ni mbaya zaidi kuwahi kutokea katika maisha yake ya ukocha.

Man City walifungwa bao 1-0 dhidi ya mahasimu wao Man United katika Uwanja wa Old Trafford katikati ya wiki hii kwenye mchezo wa Kombe la EFL.

“Goli tulilofungwa katika mchezo dhidi ya United lilitokana na mpira mrefu, tukashindwa kuudhibiti na hatimaye tukafungwa.

“Wakati mwingine unaruhusu goli kwasababu umeshindwa kuzuia mipango ya goli kama ilivyotokea kwetu na wakati mwingine unaweza kutumia pasi ndefu na ukaruhusu goli vile vile.

Guardiola alienda mbali zaidi kwa kusema: “Kwa aina ya washambuliaji tulio nao kama Kelechi, Kun Aguero, si vyema kwangu kutumia pasi ndefu, labda kwa siku zijazo nikinunua straika mwenye urefu wa sentimeta 220 nitaweza kutumia mfumo huo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here