Home Kimataifa Gor Mahia yatiliwa mashaka Confederation Cup

Gor Mahia yatiliwa mashaka Confederation Cup

3838
0

Gor Mahia imepagwa Kundi D katika makundi ya kombe la shirikisho Afrika pamoja na Zamalek, NA Hussein Dey na Atletico Petroleos.

Mwandishi wa habari za michezo nchini Kenya David Wathika anasema wakenya wengi wanaamini Gor Mahia ipo kwenye kundi la kifo!

“Kwa wadadisi wa mpira, waandishi wa habari na viongozi wa Gor Mahia ikiwa ni pamoja na Mtendaji Mkuu Lordvick Aduda wanakubaliana kwamba kuwa hili ni kundi gumu na itabidi vijana wa Gor Mahia ambao msimu huu bado hawajaonesha uwezo wa juu kama walivyozoeleka wakicheza itabidi wajitahidi kuhakikisha wanafuzu robo fainali ya mashindano hayo.”

“Msimu huu Gor Mahia imewafunga New Star ya Cameroon na hapo awali Big Bullets kutoka Malawi kabla ya kufuzu hatua ya makundi lakini mabingwa hao wa ligi kuu ya Kenya waliondolewa kwenye mashindano ya Champions League baada ya kufungwa na Lobi Stars kutoka Nigeria na kuangukia mashindano ya Confederation Cup.”

“Hivi karibuni wamemsajili aliyekuwa mshambuliaji hatari wa timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ Dannis Oliech ambaye tayari amefunga mabao matatu katika mechi tatu tanguasajiliwe kwa hiyo mashabiki wengi na maafisa wengi wa Gor Mahia wanaamini Oliech atakuwa mbadala wa Kagere.”

“Itabidi Gor Mahia ifanye kazi ya ziada ili angakau imalize katika nafasi ya pili kwenye kundi lao, ikumbukwe msimu uliopita ilifika hatua ya makundi pia na kupangwa kundi moja na Rayon Sports, USM Ulger na Yanga ambapo Gor Mahia ilimaliza katika nafasi ya tatu nankuaga mashindano huku USM Ulger na Rayon Sports zikifuzu hatua iliyofuata.”

Je, msimu huu itakuwaje katika kundi hili ambalo Gor Mahia itakuwa ikipambana na Zamalek, NA Hussein Dey na Atletico Petroleos?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here