Home Kimataifa Golden State Warriors Chali Mechi Ya Kwanza Ya Msimu.

Golden State Warriors Chali Mechi Ya Kwanza Ya Msimu.

5604
1

Wakiwa ni mabingwa watetezi huku pia wakiwa wametwaa ubingwa wa NBA mara mbili na kuingia fainali mara tatu mfululizo katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita, klabu ya Golden State Warriors ikiendelea kuwa chini ya kocha Steve Kerr ilikuwa inafungua pazia la ligi ya NBA dhidi ya Houston Rockets, alfajiri ya leo kwenye uwanja wa Orcale Arena, huko Oakland San Fransisco.

Warriors walianza kwa kuwa na sherehe fupi ya kukabidhiwa pete zao ambazo ni zawadi ya kutwaa ubingwa wa NBA. Lakini huku kwenye michezo mingine ikiwa imezoeleka kuwa na medali kwenye NBA na michezo mingi ambayo asili yake ni Marekani hutumia pete kama zawadi rasmi.

Golden State Warriors ilianza mchezo huu bila ya kuwa na nyota wake Andre Iguodala ambaye ana majeraha, lakini pia ikiwakaribisha wachezaji wapya Nick Young, Jordan Bell ambaye ni kinda kutoka chuoni na Omri Casspi.

Mchezo huo ambao ulikuwa kama sherehe ya mitupo ya pointi 3, ilishuhudia Warriors wakimaliza mchezo kwa kupoteza dhidi ya James Harden na Chris Paul ambaye amejiunga na Houston Rockets akitokea Los Angeles Clippers kwa pointi 121-122. Harden aliiongoza Houston kwa kufunga pointi 27, Erick Gordon akifunga pointi 24 na PJ Tucker akimaliza na alama 20.

Warriors waliongozwa na Stephen Curry aliyefunga pointi 22, Klay Thompson akaongeza 16, Kevin Durant akafunga pointi 20 baada ya kutokuanza vyema mchezo, huku Nick Young akimaliza mchezo na alama 23 akitokea benchi akiwa amepata mitupo 6 ya pointi 3. Draymond Green alitoka katika robo ya tatu na hakuweza kurejea kutokana na kuumia goti.

HIGHLIGHTS

 

 

Comments

comments

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here