Home Kimataifa Golden State Warriors Atokea Tundu La Sindano VS San Antonio Spurs.

Golden State Warriors Atokea Tundu La Sindano VS San Antonio Spurs.

2038
0

Warriors hakujulikana kipi wanachokifanya uwanjani mpaka pale ambapo Stephen Curry alipoanza kufanya vyema kwenye robo ya tatu ya mchezo wa kwanza wa fainali ya kanda ya Magharibi dhidi ya San Antonio Spurs, huku akimpisha Kevin Durant kuamua mchezo katika robo ya nne.

Nyota hao wawili ndio pekee ambao kwa upande wa Golden State Warriors walionekana kuwa tayari na kujiandaa vyema na mchezo wakati wenzao wakiwa wapole ndani ya uwanja.

Curry alifunga pointi 40 ikiwemo mtupo wake uliofanya matokeo kuwa sare zikiwa zimebaki dakika 1:48 na Warriors walitoka nyuma ya pointi 25 na kushinda mchezo huo lakini sababu kubwa ikiwa kuumia kwa mchezaji Kawhi Leonard aliyeumia kifundo cha mguu.

Warriors walishinda mchezo huo kwa kuwapiga  San Antonio Spurs 113-111 katika mchezo huo wa kwanza wa fainali.

“Hii ni hatuaya mtoano. Unatakiwa utegemee mambo yoyote yanayoweza kujitokeza ndani ya mchezo. Siwezi kuuita utelezi kutokana na yaliyotokea kwani ilitubidi kufanya juhudi kiufasaha pia ili kupata matokeo haya. Walikuja vyema na walifanya kila walilotakiwa kufanya na kutupa changamoto. Tunatakiwa kujifunza na kufanya vyema katika mchezo wa pili.” alizungumza Stephen Curry.

Draymond Green aliipa Golden State uongozi wa kwanza baada ya kuwa nyuma kwa takribani pointi 25.

Leonard alitoka kwenye robo ya 3 akiwa ametonesha kifundo cha mguu ambacho kilimfanya asicheze mchezo wa 6 katika hatua ya nusu fainali dhidi ya Houston Rockets, na kutoka kwake kuliwapa nafasi ya kufunga pointi 18-0.

Durant alifunga 10 mfululizo katika robo ya nne akimaliza mchezo na pointi 34 huku Zaza Pachulia ambaye alimuumiza Kahwi Leonard alimaliza na pointi 11 na kudaka rebound 9.

Leonard mpaka anatoka alikuwa na pointi 26 na kudaka rebound 8 huku LaMarcus Aldridge akiwa na kiwnago bora kabisa akimaliza mchezo na pointi 28 na kudaka rebound 8.

HIGHLIGHT

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here