Home Kitaifa Geoff Lea anaiangalia Yanga kwa jicho la tatu

Geoff Lea anaiangalia Yanga kwa jicho la tatu

5132
0

Ni vigumu sana kwa mtu anayeangalia mpira na kuufuatilia halafu haendeshwi na hisia anaweza kuipa kuipa nafasi kubwa Yanga kushinda mechi dhidi ya Simba labda kama anataka kuwaridhisha watu tu.

Bado pia nafasi ya Yanga naiona, technically mpira wa miguu unanafasi ya emotions na psychology pamoja kwamba kuna ubora form ya wakati huo na vitu vingine lakini bado nafasi ya psychology ni kubwa.

Ni rahisi sana kwa hali halisi ilivyo kuwaingia wachezaji wa Simba vichwani na kuwafanya wabweteke, siku zote hasara ya kubweteka ni kwamba ile determination ya mchezaji. Ukiachana na mchezaji kufanya mazoezi lakini usiku anapokwenda kulala anawaza kesho nacbeza na timu fulani kuna kitu fulani lazima nizingatie.

Kwenye mechi ambayo mchezaji anajua kesho anaenda kushinda, ni vigumu sana kwake kuzingatia mpinzani anaubora gani. Mahali ambapo makocha sasa hivi wanafanya maandalizi tofauti ni kwenye vitu vidogovidogo.

Ni rahisi kwa wachezaji wa Simba kubweteka kusahau vitu vidogovidogo na ni sahisi sana kwa Yanga kuzingatia kwa sababu wanaogopa kupata matokeo mabaya, wakajiandaa vilivyo dhidi ya Simba kwa mazingira ambayo mchezo unaweza kuwa upande wao.

Kwa ujumla kila kitu kipo upande wa Simba kwa sababu hata hizi mechi ambazo inacheza na AS Vita na Al Ahly halafu inafungwa zote zinaiandaa vizuri Simba kuliko Yanga. Kwa hiyo ni rahisi kwa Simba kutumia somo wanalopata kwenye mechi hizo kuelekea mchezo dhidi ya Yanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here