Home Ligi EPL Fred anaitaka United, Mwana FA kasema usije mjini

Fred anaitaka United, Mwana FA kasema usije mjini

18980
2
Nimesikia tetesi kuhusu Fred kujiunga na Man United.

Awali ya hapo sikuwa namfuatilia sana ila nimewahi kumsikia sana. Nilishindwa kuwatofautisha kati yake na Malcom. Na nilitaraji siku moja waje vilabu vikongwe tuone uwezo wao haswa. Hata hivyo klabu ya Man City pia inamuwinda kinda huyu wa kibrazili

Nasikitika kumsikia Fred anaelekea United.

Kwa nijuavyo mimi Kukaba na kushambulia ni vitu vyenye uzito tofauti kama wa shuka na Blanketi.

Ili Mourinho akusafishe mgongoni lazima usafishe sabuni kwanza. Na huwezi kumkosha Mourinho kwa chenga unazopiga ila kilometa ulizokimbia kukaba.

Fred ni kiungo mbunifu sana kuliko uwezo wake wa kukaba.
Mwana FA ni Mshabiki mkubwa wa Man United.

Leo nimebahatiki kusikiliza wimbo wake mmoja uitwao USIJE MJINI. Nimeutafakari kwa kina nimegundua kuna Mengi ya kujifunza. Hata kwa wachezaji wetu wa hapa ndani huu wimbo unawahusu sana na yafaa wajifunze kitu. Nadhani unamuona mtu kama Mo Ibrahim wa Simba, ana kiwango kikubwa sana lakini hana nafasi. Pia pale kwenye benchi la Simba kuna mtu anaitwa Said Ndemla nae maisha yake ni ya tabu kama wa wakazi wa bonde la Jangwani.

Leo hii kuna taarifa zinasamabaa Marcel kaheza nae anaenda Simba. Huyu nae namsikitikia sana.

Wachezaji wengi huwa wanapapatika kwenda vilabu vikubwa kwa sababu tu ya maslahi. Sawa wanahitaji mafanikio lakini je wataendana na mifumo ya klabu husika, Je Vipi kuhusu nafasi ya wao kucheza.

Kwa mfano tu, United ni kama Jiji, unaweza kwenda na degree yako na mambo yakaenda mrama

Fred amechagua fungu jema. Ni kweli kucheza United ni heshima kubwa. Tatizo linakuja je itadumu! Old trafford ni ardhi ya baraka na mikosi (Luis Nani)

Turudi kwa Mwana Fa.
Mwanafa anasema Ogopa matapeli nyumba hii haiuzwi.


Ninachokiamini mimi ni kwamba Moja ya nembo maarufu Man United ni kukaba.

Wachezaji wote wanataka nafasi ya kucheza kwahiyo unapaswa kupambana wala haijalishi unakipaji kiasi gani. Mourinho amekuwa akilalamikia wachezaji kila siku kama tarumbeta ya harusi kuwa baadhi ya wachezaji hawajitumi (Martial na Shaw).

Kila mshabiki wa Man United ni mchambuzi na chambuzi zao zote huwa hazifanani. Kumbuka yule Mkhitaryan, fundi wa kuasisti alivyokimbizwa kwa kushindwa kuendana na mfumo wake Man U kuna mengi braza.

Akina Mata wanakesha benchi tu, sio wote wana nafasi Man United usidanganywe sana na mpunga, muda wowote unaweza kutupwa (Di Maria). Huku huku ndipo aliopo Fellain huku Schneiderlin yupo Everton na Mourinho hataki kumwachia.

Sio wote mambo ni safi wakina Pogba wamegomewa na maisha wanaona haya watarudije Juventus na pesa walizonunuliwa.

Hakuna mshambuliaji hakuna kiungo wote kazi moja kukaba.

Mawazo yako yakufanikiwa ni moja ya mambo Martial aliyowaza akiwa Monaco. Msimu wa kwanza wa Martial United chini ya Van Gaal alipata tiketi ya kwenda Yuro na Ufaransa. Msimu huu licha ya kuwa mfungaji bora namba mbili kwenye kikosi cha United Lakini bado aina yake ya uchezaji imeonekana saa mbovu kwenye chumba cha mtihani.

Fred nae ataenda Urusi Na Brazil, tusishangae sana mwaka huu akaonekana wa gharama kama bei za supamaketi lakini msimu ujao huenda mkaanza kusema hata hatumuelewi.

Yafaa aangalie yanayosemwa na waandishi wa habari na wachambuzi. Man U kugumu unaweza kupotea muda wowote, kama hajiamini na haoni huo mfumo kama wa wamfaa asiangalie maslahi pekee tu bora asije mjini. Aende kwa Guardiola huko kutamfaa.
Maisha ya Man United ni mbinde yafaa kutumia akili ya kuzaliwa ndio ushinde. Akina Rashford wanahaso kila siku wapunguze makali ya maneno ya Mourinho kila siku.

Ukiangalia upangaji wa kikosi wa Mou utadhani Kuna wivu, chuki, ghasia, fitina. Watu wako mbio mbio kwendana na mfumo kupoteza nafasi hakuna.

Akina Ashley Young hawatosheki wanacheza kila namba wanawabania hadi wadogo zao akina Blind na Shaw. Wapo wachezaji ambao hata kwa macho ya kawaida hawakupaswa kuwa United lakini hao wamegeuka kuwa wabeba timu.

Lingard Mbwebwe nyingi chenga feki na usione tabasamu Juan Mata ukadhani ana amani.


Fred ni mchezaji mzuri sana hasa eneo la umaliziaji na ana kasi jitihada pamoja na nguvu. Bila shaka anafanana uchezaji wake kama wa Sanchez. Lakini je ujio wa Sanchez umeonesha tija gani katika mfumo wa toto futbo (kukaba wote) ya Mourinho?
Lakini pia anaweza kwenda tu kama mbwai iwe mbwai, Mourinho ni kama Kuni na kukaba ni moto sikutishi lakini United hapakufai. Pogba hachezi tena kiungo mshambuliaji anacheza kiungo mkabaji ashaiba dili la Herrera mji ulivyokuwa nishai.
Nafuu huko alipo Maana anaheshimika aina yake ya uchezaji. Mourinho huwa hajali kipaji ila jitihada na kumsikiliza yeye tu. Mourinho anachokihitaji ni timu kutokuruhusu bao kwanza. Hayo Mengine baadae.
Fred anakwenda Old Trafford akijua wazi kuwa Micky, Mata, na Martial pamewabumia huku aina yake ya uchezaji inawafanania.
Usishangae kichwa cha habari. Muziki wetu umekuwa. Hata hivi majuzi nilimuona Lovren akicheza wimbo wa Chegge.
Simkatazi wala siwezi kumkataza mimi muongeaji tu. Wala sina leseni ya ukocha ni mawazo yangu tu. Yote kwa Yote kila la kheri kwake.
Makala hii Imeandaliwa na Privaldinho unaweza pia kunifollow insta kwa jina hilo hilo.

Comments

comments

2 COMMENTS

  1. Ile stori ya ibra imeishia njiani kaka…tupe na wanaokukosoa wala usife moyo hao ndio wanakufuza na kukupa maarifa zaidi …

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here