Home Kimataifa EXCLUSIVE: Ambokile atua Sauz kusaini Black Leopards 

EXCLUSIVE: Ambokile atua Sauz kusaini Black Leopards 

5228
0

Mshambuliaji wa Mbeya City Eliud Ambokile ameondoka leo kwenda South Afrika kufanya mazungumzo ya kujiunga na Black Leopards inayoshiriki ligi kuu (PSL).

Awali Ambokile alienda Misri kufanya mazungumzo kwa ajili ya kujiunga na klabu ya El Gouna lakini hawakufikia makubaliano kutokana na sababu za kimaslahi.

Michael Mwebe, mratibu wa kampuni ya Siyavuma Sports inayomsimamia Ambokile amethibisha kuwa mchezaji huyo tayari yupo South Africa kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuijiunga na Black Leopards.

“Ambokile ameondoka leo kwenda South Africa kufanya mazungumzo ya kujiunga na Black Leopards. Kufikia jioni mambo yanaweza kuwa mazuri.”

Mwebe amesema pia deal la kujiunga na El Gouna lilikufa kutokana na sababu za maslahi.

“Mambo yalishindikana huko (Misri) kwa sababu za maslahi.”

Black Leopards inafundishwa na Dylan Kerr, kocha wa zamani wa Simba na Gor Mahia ya Kenya.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here