Home Kimataifa Eto’o ashtakiwa kwa kutelekeza mtoto

Eto’o ashtakiwa kwa kutelekeza mtoto

4386
0

Nyota wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o anatarajia kupelekwa mahakamani na mwanamama Adileusi do Rosario Neves kwa madai kuwa amemtelekeza mtoto wake.

Neves anasema wakati Eto’o akiwa anachezea Leganes alizaa nae mtoto ambaye kwa sasa ana miaka 19.

Lakini Eto’o hakuwahi kumtambua mtoto huyo anayejulikana kama Erika.

mwanasheria wa mwana mama huyo amesema tayari kesi imeshafunguliwa jijini Madrid na itasikilizwa tarehe 24 mwezi April mwaka huu.

Mwanamama huyo amedai kuwa walianza mahusiano yao ya siri na Eto’o mwaka 1997 wakati Eto’o akiwa anacheza kwa mkopo ndani ha klabu ya Leganes akitokea Madrid.

Neves ni mzaliwa wa Cape Verde anadai baadae aligundua kuwa yeye ni mjamzito ambapo alijifungua mwaka 1999.

Mahakama itaamuru vipimo vya DNA kufanyika ili kujua ukweli wa suala hilo.


Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here