Home Kitaifa Eneo gani uwanjani litaamua mechi ya watani wa jadi?

Eneo gani uwanjani litaamua mechi ya watani wa jadi?

4383
0

Shaffih Dauda

Naiona mechi ikiamuliwa katikati ya uwanja (eneo la midfield) Simba ni timu inayicheza mpira kuanzia nyuma wanapiga pasi na kutawala eneo la katikati.

Changamoto inayokuja kwa timu pinzani ni kuizuia timu inayocheza kwa style ya Simba ni kushindana katika kupokonya mipira lakini ukishindwa kuwanyang’anya mpira ili kutekeleza mipango yako, inamaana utakuwa umeshindwa.

Nikiangalia hii mechi on papers kwa pande zote mbili, wachezaji wanavyocheza, naiona Simba itatawala eneo la katikati ya uwanja eneo ambalo litaamua matokeo mchezo wa Yanga vs Simba.

Simba kama itatawala eneo la katikati basi inanafasi kubwa ya kushinda na sehemu ambayo itaweza kuwanyimba Simba jinsi ya kushinda ni Yanga wakifanikiwa kushindana na kuwashinda Simba kwenye eneo la kiungo ambalo ni silaha kubwa ya Simba.

Geoff Lea

Mimi natofautiana na Dauda, sio kweli kwamba timu ikiwa haina midfield nzuri haiwezi kushinda dhidi ya timu yenye midfield nzuri. Makocha ambao ni wabunifu wanaweza kukiona na kuna njia ya kucheza dhidi ya timu yenye midfield wazuri.

Inawezekana Yanga wanajua Simba wana viungo wazuri hivyo Yanga wakaamua kupitisha mipira mirefu, hakuna pasi fupifupi kwenye eneo la katikati.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here