Home Kimataifa “Eden Hazard asepe tu” Sarri

“Eden Hazard asepe tu” Sarri

6243
0

Kocha mkuu wa Chelsea amesema hana muda wa kuzuia wachezaji wanapohitaji kuondoka.Kwa kipindi kirefu Hazard amekuwa akihusishwa na miamba ya soka Hispania Real Madrid.Chelsea kwa kipindi cha hivi karibuni wamekuwa kwenye hatakati za kutaka kumuongezea mkataba mpya bila matunda yeyote.Kocha huyo hivi majuzi alimkatalia Odoi kujiunga na klabu ya Bayern Munich.”Odoi haendi popote labda asubiri dirisha kubwa la usajili mwezi julai” Sarri.Kuhusu sakata la Hazard Sarri ametolea ufafanuzi.”Hazard ana miaka 28, kama anataka kuondoka aondoke tu” Sarri.Hapo awali pia Sarri aliwahi kuongelea kiwango cha Hazard ndani ya klabu hiyo.”Hazard ni mbinafsi sio kiongozi mzuri”Lakini Hazard nae hakukaa kimya alijibu kauli kwa kusema“Sipendi kuongea sana, huwa nafanya kazi niliyotumwa kufanya basi mengine hayanihusu. Kuna watu wameumbwa kubweka ila mimi naongea na mpira.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here