Home Ligi BUNDESLIGA Dortmund Wachukizwa na Mitindo Ya Nywele Ya Aubameyang Kwa Masuala Ya Udhamini.

Dortmund Wachukizwa na Mitindo Ya Nywele Ya Aubameyang Kwa Masuala Ya Udhamini.

5781
0

Borussia Dortmund wamesema watazungumza na Pierre-Emerick Aubameyang baada ya kuonekana akiwa ameweka mtindo wa nywele ambao ulikuwa na ishara ya kuonyesha alama ya Nike ambao ni wadhamini wake binafsi kwenye mchezo dhidi ya Bayer Leverkusen.

Aubameyang kwenye nywele zake alionekana kuwa na alama ya pink ya kampuni ya Nike kwenye ushindi wa mabao 6-2 ambapo mshambuliaji huyo wa Gabon alifunga goli lake la 20 na 21 la msimu huu.

Puma wadhamini na wanahisa wa klabu ya Dortmund na ndio wazalishaji wa jezi zao, ambapo mkurugenzi wa kiufundi wa klabu ya Dortmund, Michael Zorc ameweka wazi kuwa hawataki hilo litokee tena.

“Hii pengine imetokana na udhamini wake binafsi wa Nike, kama nitakuwa nimeelewa vyema,” Zorc aliiambia¬† Sky. “Hii tunaamini haitojirudia baada ya kujadili nae tukishaketi.”

Dortmund bado hawajampa adhabu au kupiga faini Aubameyang baada ya tukio hili na hawajaweka wazi kama watafanya maamuzi yoyote dhidi yake.

Magoli mawili ya Auba yalimfanya aongoze mbele ya straika wa Bayern Munich, Robert Lewandowski kwenye mbio za kuwania ufungaji bora wa ligi kuu ya Bundesliga maarufu kama Torjagerkanone.

Aubameyang pia amempita Lewandowski kama mfungaji bora wa Borrussia Dortmund wa muda wote kwenye orodha ya wafungaji wa klabu hiyo. Mpaka sasa ameshafunga mabao 75  kwenye michezo 118 ya Bundesliga kwa Dortmund huku Lewandowski akiwa amefunga mabao 74 kwenye michezo 131 kwa kipindi cha mwaka 2010 mpaka 2014.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here