Home Ligi BUNDESLIGA Dili 10 kubwa zinazoweza kufanyika United, Chelsea na Madrid kabla ya mwisho...

Dili 10 kubwa zinazoweza kufanyika United, Chelsea na Madrid kabla ya mwisho wa dirisha la usajili

17012
0

Zimebaki siku 10 tu kwa dirisha kubwa la usajili barani Ulaya kufungwa, usajili wa safari hii umeonekana sio wa mbwembwe sana tofauti na uliopita. Lakini bado katika siku hizi 10 kuna dili zinaweza kukamilika.

Aaron Ramsey – Chelsea. Wengu hawalioni hili ila mkataba wa Ramsey na Arsenal umebaki mwaka mmoja tu na hakuna dalili ya mazungumzo, Chelsea wanaiwinda saini yake na ujio wa Maurizio Sarri unaweza kumshawishi Ramsey kusaini The Blues.

Thibaut Courtois – Real Madrid. Tetesi za Courtois kwenda Madrid zilikuwepo tangu kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa, Madrid wanajaribu na japo imekuwa ngumu ila inaonekana kuna asilimia nyingi ya usajili huu kutokea.

Willian – Manchester United. Usajili wa Malcolm kwenda Barcelona umekatisha habari za Wilian kujiunga na Barca, na sasa Manchester United na kwa mbaali Real Madrid ndio ambao wanapewa nafasi kumnunua Willian.

Eden Hazard – Real Madrid. Binafsi siamini kama Real Madrid watamaliza dirisha hili la usajili bila kununua nyota mkubw, hadi sasa hawana usajili mkubwa waliofanya japokuwa Cr7 ameondoka na wanaonekana labda wanajiandaa na jambo kubwa, Hazard mwenyewe anaonekana kupendezwa na tetesi hizi na hili linaweza kutokea mda wowote.

Harry Maguire – Manchester United. Inatajwa kwamba inahitajika karibia £60m kumtoa Maguire Leicester City, United wamemuweka huyu katika orodha ya juu kabisa ya nyota wanaowataka na labda katika siku hizi 10 wanamaliza jambo lake.

Christian Pulisic – Chelsea. Borussia Dortmund wanasema hauzwi lakini wakala wake ameshakutana na wakurugenzi wa tinu mbali mbali ikiwemo tajiri wa Chelsea Roman Abromovich, kuna uwezekano Abromovich akatumia ushawishi mkubwa alionao kumpata Pulisic.

Alvaro Morata – Juventus. Majuzi tu Maurizio Sarri alikiri kutoridhishwa na kiwango cha Morata, lakini bado anampa muda. Kama Chelsea watafanikiwa kuoata mshambuliaji mpya baasi ni wazi Morata atakuwa njiani kuondoka Chelsea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here