Home Kimataifa Dauda vs Geoff Lea & Maeda kuhusu Barca kumsajili Boateng

Dauda vs Geoff Lea & Maeda kuhusu Barca kumsajili Boateng

4134
0

Baada ya Barcelona kumsajili Kevin Prince Boateng raia wa Ghana, mijadala imekuwa mingi sana kila mmoja akiwa na mtazamo wake binafsi.

Swali kubwa linaloulizwa ni je Barcelona wameshindwa kuendeleza utamaduni wao uliodumu kwa muda mfupi wa kutumia wachezaji wanaowaandaa kwenye academy yao ya La Masia?

Jana kupitia Sports Xtra mimi pamoja na wenzangu Issa Maenda na Geoff Lea kila mmoja alitoa maoni yake kuhusu usajili huu wa Boateng.

GEOFF LEA

Mimi sidhani kama Barcelona walikuwa wanamuhitaji sana Boateng labda kama kuna vitu vya kipekee sana ambavyo kocha au benchi na ufundi la Barca walikuwa wanavitafuta kutoka kwake kwa sababu kama tunazungumzia nafasi yake ya uchezaji, jamaa ni kiungo mshambuliaji na sifa zake au uchezaji wake anamchango sana kwenye eneo la ushambuliaji ukiangalia Barca ina washambuliaji wengi ukianzia na akina Messi, Suarez, Dembele mtu kama Coutinho na wengine.

Eneo la katikati kuna akina Vidal, Rakitic na wengineo, mimi sishawishiki sana kwamba Barcelona walikuwa wanamuhitaji sana Boateng lakini linapokuja suala la umri wake na profile yake kama mchezaji ndio yanaibuka maswali mengi kuliko majibu kwenye huu usajili.

ISSA MAEDA

Mimi naona Barcelona walikuwa wanahitaji sana mtu wa kumsaidia Busquet kwa sababu huwa wanapata tabu sana kila wanapomkosa kwa sababu aina ya watu wao wanaocheza eneo la ushambuliaji, wapo wengi ukiachana na Boateng kuongezeka lakini wengi hawapati nafasi kwa mfano Arthur Henrique hatumiki mara kwa mara, Coutinho amepoteza nafasi kwenye kikosi labda kuna kitu ambacho mwalimu amekiona kwake ambacho sisi hatukioni kwa jicho la kawaida.

SHAFFIH DAUDA

Kinachosababisha mtu asajiliwe ni uhitaji, benchi la ufundi kwa kuangalia sera ya klabu (vilabu vilivyoendelea, vinasajili wachezaji ambao wanaingia kwenye aina yao ya uchezaji) ukiangalia Barcelona ya zamani chini ya Johan Cruyff alikuwa anaamini zaidi wachezaji kutoka academy yao ya La Masia ambayo yeye ndio alikuwa mwasisi.

Nyakati zinabadilika, bahati mbaya tupo kwenye dunia ambayo haikusubiri kumwandaa mchezaji, dunia ya sasa mahitaji ni ya papo hapo kwa hiyo utaangalia mwenye umwandae mtoto wako halafu umpe nafasi akuthibitishie ubora wake au wakati unamwandaa ukubali kutumia wengine ambao walishaiva.

Kizazi cha akina Puyor, Iniesta, Xavi, Pique kimeondoka maana yake wanatakiwa wawainginze watoto wengine wawaamini lakini wengi wa vijana waliopikwa La Masia wanaondoka kwenda sehemu nyingine.

Tunatakiwa kujiuliza kwa nini wanaondoka? Je hawakuwa na uwezo wa kuvaa viatu vya hawa walioondoka? Jibu ni hapana, hawajaaminiwa na kupewa muda kwa sababu hata akina Xavi na Iniesta wanaingia walikuwepo akina Edmilson, Guardiola, Riquelme lakini sasa hivi hakuna muda wa kusubiri unahitaji watu ambao wamesha-prove waje upate matokeo.

Lakini wanasajilije hapo ndio kuna mjadala mwingine kwa sababu ukiangalia katika kipindi cha mwaka 2014 hadi kabla ya dirisha hili la January walikuwa wamesajili wachezaji 22 ambapo 12 kati ya hao waliondoka baada ya kukosa nafasi.

Mwaka 2014/15 Suarez, Stegen, Rakitic, Vermaelen waliingia na wameendelea kuwepo walioondoka Mathew, Bravo na Douglas 2015/16 Turan akasajiliwa, unajua walipo sasa hivi?

Boateng ni mchezaji mzoefu kacheza EPL, Bundesliga, Seria A, La Liga, timu ya taifa kwenye michuano mikubwa kama kombe la dunia na mataifa ya Afrika kwa hiyo Barca ndani ya January hii wanataka mtu ambaye tayari ameshathibisha ubora wake bila mashaka yoyote kwa hiyo wanataka mtu ambaye anauwezo wa kucheza timu kubwa wanamleta ili acheze kwa muda mfupi wapate wanachokitaka.

Kwa mtazamo wako nani kati ya Geoff Lea, Issa Maeda na Shaffih Dauda nani yupo sahihi?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here