Home Kitaifa Dar City yamkomalia mchezaji Yanga

Dar City yamkomalia mchezaji Yanga

3567
0

Mchezaji Gustapha Saimon Lunkombi ambaye usajili wake umezua utata baada ya kuitumikia Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Singida United, ishu yake imezidi kuwa na sura tofauti.

Klabu ya Singida United iliibua mjadala baada ya kutuma malalamiko TFF kwamba Yanga imemtumia mchezaji huyo ambaye ni mchezaji halali wa Dar City FC ya Ilala, Dar es Salaam.

Rais wa Dar City Azim Khan amesema mchezaji Gustapha Khan ni mchezaji wao halali na mkataba wao na mchezaji unatarajiwa kumalizika mwezi wa 7 mwaka huu.

Gustapha amekuwepo Dar City kwa muda gani na ameondokaje kwenda Yanga?

“Gustapha Saimon ni mchezaji wetu tulikuwa naye tangu mwaka 2016, timu ilipoanza kwenda Kanda kule Kahama tulikuwa nae na baadaye tulivyokosa nafasi Kahama tukamsajili tena katika timu ya Pepsi ambayo tuliinunu sisi Dar City mwaka 2017/18 ikiwa daraja la pili na tukamtumia mchezaji Gustapha.”

“Tukacheza ligi daraja la pili Taifa tukafanikiwa kupanda ligi daraja la kwanza tukabadilisha jina tena kurudi kuwa Da City tukasaini nae tena mkataba, akasaini payment voucher vitu vyote tunavyo sisi.”

Mkataba mliosaini na Gustapha ni wa muda gani?

“Amesaini mkataba tarehe 15 July 2018 na unaisha tarehe 14 July 2019.

Kwa nini Gustapha yupo Yanga?

Yeye na Yanga wanafahamu zaidi kwa nini wamemchukua mchezaji wetu labda kutokana na ubora wake wameona atawafaa lakini hawakufuata taratibu.

Mliwafuata Yanga baada ya kumuona mchezi wenu yupo kwao?

Tuliwajulisha kupitia makamu wangu wa Rais aliwapa taarifa lakini Yanga hawakujibu na waliendelea kumtumia mazoezini na mechi za kirafiki lakini sisi tuliendelea kuamini kwamba ligi itakapoisha msimu huu watasubiri usajili utakapofunguliwa wamsajili kihalali lakini tumeshangaa kumuona kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida United.

Inaonekana Gustapha ana leseni mbili, imekuwaje akawa na leseni hizo?

Sisi tunayo leseni yake tangu mwezi wa 8 mwaka jana kama sikosei mpaka leo leseni yake bado tunayo. Sasa hilo swali nadhani waulizwe TFF mimi siwezi kulijibu.

Mmeshapeleka taarifa TFF kuhusu hiki kinachoendelea?

Tayari tumepeleka malalamiko TFF tukiwa tumeambatanisha vielelezo vyote tunasubiri majibu.

Mna vielelezo gani kwamba Gustapha ni mchezaji wenu halali?

Sisi tuna mkataba original, tuna payment voucher ambayo amesaini anapokea fedha kutoka kwetu, tuna cheti cha kuzaliwa na leseni yake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here